Good Morning mtu wangu, leo ni Alhamisi 29 October 2015, na kama ilivyo kila siku lazima tuanze na uchambuzi wa magazeti, jukumu langu ni kuzisogeza kwako zile zote kubwa za leo kwenye kuperuz na kudadisi…
Uchaguzi Zanzibar wafutwa, ZEC yasema kuwa Uchaguzi Mkuu haukuwa na haki kutokana na kutokufuata taratibu na Sheria, Wagombea Urais CCM, UKAWA wazidi kuchuana matokeo ya Urais Uchaguzi Mkuu 2015, Edward Lowassa ataka matokeo ya Uchaguzi Mkuu kusitishwa na kusomwa upya huku NEC yapinga yasema matokeo yanayotangazwa ni halali.
Matokeo ya Ubunge Mbagala bado ni giza nene, kundi la watu linalodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Siasa wachoma ofisi ya ofisa mtendaji, Moshi kwa madai ya kutoridhishwa na matokeo ya udiwani baada ya ofisi hiyo kutangaza matokeo ya ushindi kwa Chama cha upinzani… CCM kupinga Mahakamani matokeo ya majimbo manne baada ya kutoridhishwa na ukusanyaji wa matokeo kwenye majimbo hayo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC imetangaza majimbo 153 yalioongoza kwa kutokuharibu kura kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika October 25 2015, baadhi ya majimbo hayo ni Jimbo la Mkwakwa, Jimbo la Kilindi, Jimbo la Lupembe, Jimbo la Madaba, Jimbo la Monduli na Jimbo la Mwangwa… UKAWA washinda kata nyingi jijini Dar es salaam hivyo kuwawekwa kwenye nafasi nzuri ya kuuongoza baraza la madiwani na kwa mara ya kwanza kuwa na nafasi kubwa ya kuongoza halmashauri ya Dar es salaam.
Mgombea Urais nchini Ivory Coast, Hassan Watara ameshinda Uchaguzi Mkuu nchini humo kwa wingi wa kura za 83.66% … Kituo cha Uangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu nchini, SIMOT leo kutoa taarifa ya jumla ya tathmini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyikaOctober 25 2015
Post a Comment