Social Icons

Loading...

MAHABA NIUE...STORY YA KUSISIMUA...

MAHABA NIUE...(49)
AGE...(18+)
Mtunzi..EMMANUEL F. KWAY
0718 862176
ILIPOISHIA.
Mwasha aliongea kwa hasira huku akiweka bastola yake kiunoni na kutoka njee na kuingia na watu wake ndani ya gari, na safari ya kwenda Sinza kumkamata Ramsey kuanza....
TWENDE KAZI..
"hivi mke wangu nini ulikosa kutoka kwangu?'"
aliuliza Mr, mwasha akiwa siti ya nyuma ambapo alikaa kati kati kushoto alikaa Naike na kulia kwake alikaa josephime mke wake huku mbele akiwa amekaa kijana wake pamoja na dereva, vile vile nyuma kulikua kuna gari nyingine ya watu wake iki wafuata,
kweli Mr, mwasha kitendo cha kumegewa mke wake kili muuma sana, mwana mke ambae alimuamini pengine kuzidi hata Mama yake mzazi aliye mbeba miezi tisa tumboni.
mwanamke ambae alipewa kila aina ya vitu vya thamani leo hii ana shindwa kuamini kilicho tokea, hakuwahi kuwaza kama ipo siku mke wake atakuja kumsaliti na kumvulia nguo mwanaume mwingine ili kua ni aibu sana na fedhea hasa kwa watu waliojua wadhifa wake.
"nisamehee mume wangu!."
"nime kuuliza swali, kipi kili kufanya utembee na yule kijana"?
"ni shetani"
Mr, mwasha alitupa kofi aina ya kelbu lililo tua juu ya mdomo wa JOsephine na kumfanya aanze kulia kwa uchungu, kweli alijutia kitendo cha kumsaliti mume wake, hakustaili kusalitiwa, hakustaili kumvulia chupi Ramsey ambae leo hii vile vile alikutwa na mwamke mwingine gest,
wakati huo Naike alikua akilia machozi sana, hakuelewa nini hatma yake, hakuelewa mwisho ungeishia vipi, safari
nzima alikua akilia kwa kwikwi akiomba msamaha sababu hakujua nini kinaendelea na kutojua watu wale ni akina nani, fikra yake ili mtuma kuwa wale watu ni hatari sana ni wabaya, ila maongezi aliyokua akiongea mwasha yali fanya apate picha na kuanza kujua kila kitu,
"mke wangu, nime kupa gari nzuri ya kutembelea,kampuni nime kukabidhi nzuri, haya ndo malipo!, siku tegemea kabisa, ona navyo aibika leo hii, ona unavyo dhalilika , hivi Enock akijua izi habari unadhani ata kuchuliaje, si atakudharau, naongea nawewe malaya mbwa, Hivi ulikosa nini kwangu, yaaani....."
Mr, mwasha aliongea kwa hisia kali hasa huku machozi ya hasira yaki mlenga lenga, moyo wake ulimuuma sana kupita kiasi, alihisi kama mkuki umetua ndani ya moyo wake tena wenye moto, na kuapia endapo ata muweka Ramsey mikononi ata mfanya kitu kibaya kabla ya kumuuwa,
tayari gari izo zili fika maeneo ya shekilango likikata kona, kuelekea sinza
"sikia Abubakari, usifike pakistani kabisa, uta simama mbali kidogo na hiyo sehemu, alafu huyu binti ashuke, binti naomba usiende kinyume, maana nita kuua, usalama wako wa kuishi upo mikononi mwako sasa hivi!, mwenyewe uta chagua kifo au uhai"
"ni mekuelewa"!
"nataka Ramsey nimkamate, endapo utafanya makosa yoyote yale, wewe uta chukua adhabu ya RAmsey"
aliongea Mr, Mwasha huku akimtolea macho Naike, kweli yalikua ni maneno ya kutisha sana, yalikua ni maneno ya kuogopesha kupita maelezo, Naike jasho lilianza kumtoka na kuwa na wakati mgumu sana, ila hakuwa na jinsi alichotaka yeye ni kuya nusuru maisha yake ni si vinginevyo,
"nakuhakikishia nita fanya ivyo, kwani mta mfanya nini"?!
"hili swala, sio kazi yako"
"sawa"
gari lili egeshwa mbali kidogo na pakistani huku waki angalia huku na kule pande zote na kumwambia Naike apige simu kwa Ramsey,
kweli jambo lile lili fanyika huku akiwa amewekewa bastola shingoni, ki ukweli alitamani sana amwambie RAmsey ukweli kuwa kitendo cha kukubali kuja waonane kinge mgharibu maishani, pengine angepoteza uhai wake, ila hakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kutekeleza amri ambayo iliambatana na bastola shingoni,
"sawa Naike baby wangu, mimi nisha fika nakusubiri mrembo"
"poa poa nakuja sasa hivi"
"usi chelewe sasa, nita fute Room"?
swali lile aliuliza Ramsey ambapo sauti yake ili sikika na kila mtu ndani ya gari lile mpka kwa Josephine vile vile, mr, mwasha ali mkata jicho kali Naike baada ya kumuona ana sua sua, na kumpa ishara ya kutingisha kichwa kuwa akatae,
"NOO usi tafute, tafuta baa yoyote ile nzuri, mimi nita kuja baby, fanya ivyo my boo"!
"okay Love, nipo hapa MANDELA PUB, njoo ukiulizia uta elekezwa"
"sawa , nita kukuta hapo"
simu ile ili katwa na kuanza kupanga mikakati ya kumnasa Ramsey..roho ya huruma ili muimgia sana Josephine maana alimpenda sana kutoka moyoni licha ya kwamba alikutwa na mwanamke mwingine lakini, alimuonea huruma sana sababu alimjua sana mume wake ni kiasi gani ana hasira mbaya sana.
alijua tayari umauti wa Ramsey una kalibia na wala si vinginevyo, hakuwa na matumaini tena juu ya maisha ya RAmsey, alimkumbuka vizuri kijana Matto ambae aliuwawa na mwasha kwa kitendo cha kumtaka kimapenzi baada ya kukuta meseji ndani ya simu yake.
huyo alipigwa risasi tatu za utosi na askari kuhongwa pesa nyingi sana kuzima kesi ile wakisingizia kuwa alikua ni jambazi,
aliamini vile vile kwa Ramsey ndicho kitakacho enda kutokea na wala si vinginevyo
"kacha kacha"
Mr mwasha alikoki bastola yake na kuiweka kiunoni na kushuka na Naike ndani ya gari,
"Abubakari shuka, nenda na huyu binti, kuwa makini nae, binti Naike, sijui Naiko what ever, kama tulivyoongea maisha yako unayo mikononi, USINIJARIBU, NITAKUUA NA sito pelekwa popote pale, umenielewa?"
"ndio!"
yalikua ni maneno ya kutisha sana kwa Naike,NA kumfanya AANZE kulia tena machozi,
"Abubakari, akifanya ujinga, piga piga sana, alafu nakuja kumaliza mimi, Namtaka huyo kunguni Ramsey nakuhesabia"
"sawa bosi, nipe dakika sifuri hiyo ni kazi ndogo kama , kuua kunguni"
kweli aliloliongea mwasha lili fanyika hakuwa katika sura ya utani hata kidogo, alicho taka siku zote kili tendeka mara moja, Abubakari na Naike waliongozana wote..
*********
Ramsey akiwa amekaa kwenye kiti na bia ya Serengeti mezani akimsubiri Naike kwa muda mwingi sana.bila kujua kina choendelea. aliangalia saa yake ya mkononi na kuona muda una zidi kwenda,, baada ya sekunde chache simu yake inaita na kuona ni prosper akipiga,
"oyaa yule demu yupo dukani hapa,"!.
"demu gani huyo tena P"?
", yule Martha ana taka simu yake, sasa sijui ulipo iweka"
"mwambie baadae au aje kesho"
"Ramsey njoo sasa hivi, mi ana ni sumbua, njoo mara moja ndo urudi uendelee na mambo yako"
"mwambie asubiri, kama hawezi arudi kesho"
"shika huyu hapa ongea nae"
"kaka jamani, naomba ile simu pesa yako nishaleta"
"sikia samahani dada angu, mimi nipo mbali sana nipo kibaha, njoo baaadae au kesho"
"jamaniiiii, jaamaaani"
"ndo ivyo, ile simu ipo home"
"basi nita kuja kesho, ila sija penda, sijapenda kabisa"
"njoo kesho"
Ramsey alivyoona vile alikata simu ili kuepusha kelele zile bila kujua kuwa ni Mungu au malaika alitaka kumnusuru katika balaa linalokuja mbele yake, laiti ange jua kuwa ana tafutwa sana ange inuka mara moja na kukimbia mbio,
za ajabu.
hakuelewa kina choendelea, yeye alicho fikiria kichwani ni kufanya ngono na Naike bila kujua kuwa demu huyo alitumiwa kama chambo na mr, Mwasha.ili yeye akamatwe,
kwa mbali sana alimuona Naike akija taratibu sana akiwa mnyonge na mpka kusogea meza yake ilipo.
"vipi Naike mbona mpole sana?"
"Ramsey"
"naam Beibe"
"kimbia,"
"mbona sikuelewi, nikimbie vipi tena, ?"
"ramsey kimbia, kimbia sasa hivi"
"wewe Naike ume changanyikiwa nini?!, upo sawa kweli, nisha tafuta chumba tayari, twende tukamalizie CONDOM tayari ninazo hapa, boxi tatu nime nunua"
"Ramsey naomba ukimbie tafadhali"
"una nini binti, au ndo mapepo, acha utani wako,"
Naike alizidi kusisitiza kwa sauti ya chini sana na kumfnya RAmsey asijue kina choendelea,
laiti ange msikiliza kwa makini na kuelewa wenda ange ruka huo mtego
"Naike, niangalie nikimbie wap..."
kabla ya kumalizia maneno tayari alishikwa shati na kijana ambae haku mtambua na kuinuliwa.
"blazza vipi, mbona tuna haribiana starehe?, mbona ivyo, mimi sitoki nae huyu,, blaza vipi tena, Naike huyu kaka yako au"?
"Twende"
Ramsey alipigwa kofi zito juu ya shavu na kumfanya atulie, ki ukweli hakuelewa kina choendelea alijua wenda ni kaka yake na Naike au bwana ake ila aliburuzwa kwa nguvu sana huku akijaribu kupambana na jitu lile,
ila kijana yule alimzidi nguvu
Naike alilia machozi alijua nini kinaenda Kumpata RAmsey, alijua ni umauti na wala si kitu kingine, ila alishukuru kuokoa maisha yake kwa wakati ule..
Licha ya kushukuru ila bado katika nafsi yake alisononeka sana kitendo cha kuumuza RAmsey, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuokoa maisha yake ambayo yalikua mikononi mwake mwenyewe!
Ramsey aliburuzwa mpaka kwenye gari aina ya jaguar, gari hilo alili tambua sana nyuma ya gari hilo kulikua na BMW X5 aliya tambua magari hayo, haya kua mageni machoni mwake, licha ya kuya jua lakini bado hakuelewa nini kina endelea mpka alipoona sura ya mr, Mwasha iki tokeza ndani ya gari, na kuishiwa nguvu, kweli nguvu zili muisha na kujua si kitu kingine bali ni kifo ndo kina fuata,
Mr, mwasha alimfuata RAmsey na kumzaba kofi zito ambalo alimsindikiza na ngumi nzito ya tumbo,
"muingizeni kwenye buti, fanyeni haraka. Ramsey, naenda kukuuua, yaani wewe wa kunkumbatia  mke wangu., leo ndo leo.?"
mr, Mwasha aliongea na kumpiga tena ngumi mdomoni nzito na kumfanya Ramsey avuje damu mdomoni kutokana na kuung"ata ulimi wake,
ITAENDELEA..
bila kusahau kushea stori hii na kutembelea page yangu facebook inayokwenda kwa jina la
Story za KWAY





author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top