Mpendwa msomaji katika ushauri,mikasa na stori tamuu,
Leo ebu tujaribu kuangalia na kujadili pale Unapompenda mtu
kwa nguvu zako zote kumbe kwa upande wake ana mtu anayempenda zaidi,Tumsikilize
mwenzetu akitusimulia story fupi iliyomkuta katika mahusiano,
Habarini za muda huu MABEUTY NA MAHANDSOME,Kwa jina naitwa
Kitoi,nilikuwa na mpenzi wangu niliyempenda sana ,dada huyu kwa jina aliitwa Glady,kiukweli
tulikutana sokoni katika biashara ndogo ndogo,siku ya kwanza kabisa tulikuwa
tunasumbuliwa na wakata ushuru kuhusu kodi za bidhaa,kwa bahati mbaya au nzuri
mimi nlikuwa sina ela,hivyo basi ilibidi wachukue mzigo wangu,kumbe kwa pembeni
kuna dada alisimama ambaye alivaa kiheshima na alionyesha mstaharabu,nikiwa
sijui hili wala lile baada ya mzugo wangu kuchukuliwa nlisikia sauti
“Samahani kaka,mbona wamechukua mzigo wako?” nilijikuta najibu kwa kuropoka
bila kujali nani kaniuliza
“Eti sina ela ya ushuru nimewaambia wasubiri niuze
nitawalipa hawaelewi” Dada Yule akaniambia twende nikakulipie alafu ukishauza
utanirudishia ela yangu,nilikubali na
nilimshukuru sana.
Baada ya biashara kuisha tukiwa hata hatujajuana majina, nlimfuata Yule dada
nikamwambia
“Samahani dada yangu,nashukuru sana kwa kunilipia ushuru
asubuhi,japo ulinilipia sh.1000 naomba nikuongezee sh.500 ya shukrani” Dada Yule
akatabasamu na kuniambia
“Usijali kaka yangu,sisi wote hapa ni watafutaji,leo
nimekulipia na hata usinirudishie ila la muhimu ukija sokoni uje na ela ya
ushuru si unawajua hawa best” Aliongea huku akitabasamu na kucheka,nilimshukuru
na kuondoka,nilitaka kumuuliza jina lake ila moyo ukasita tukabaki kuitana best
kila mmoja ila kwa bahati nzuri pale kwenye kibanda chake aliweka namba za simu
ila sikuwa na uhakika kama ni zake au lah…nilizichukua na usiku nikiwa nimelala
nikasema acha nimshukuru kwenye simu…nilipiga simu na sauti iliita kwa muda
bila kupokelewa ilikuwa kam amida ya saa mbili za usiku,ghafla ikapokelewa na
sauti ya kiume …Itaendlea kesho usikose…
Post a Comment