Klabu ya FC Barcelona usiku wa October 17 ilishuka dimbani kucheza mechi yake ya Ligi Kuu Hispania kwa kuwakaribisha Rayo Vallecano katika uwanja wao wa nyumbani waCamp Nou. Licha ya FC Barcelona kushuka dimbani bila nyota wake Lionel Messi ambaye anauguza jereha la mguu wake, FC Barcelona imeibuka na ushindi.
FC Barcelona imeibuka na ushindi mnono tofauti na wengi walivyotegemea kwani kumkosa nyota wake Lionel Messi kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kudhoofisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika, klabu ya FC Barcelona iliibuka na ushindi wa jumla ya goli 5-2.
Neymar ndio aliibuka nyota wa mchezo huo kwa kufunga magoli manne kati ya matano,Neymar dakika ya 22 na 32 alifunga goli mbili kwa mikwaju ya penati kabla ya dakika ya 69 na 70 kufunga magoli mengine mawili, mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarezalihitimisha idadi ya magoli matano kwa kufunga goli dakika ya 77. Rayo Vallecano licha ya kuwa wa kwanza kufunga goli wameishia goli 2 zilizofungwa na Javi Guerra dakika ya 15 na Jozabed dakika ya 86.
Matokeo ya mechi nyingine za Laliga zilizochezwa October 17
Post a Comment