Ligi Kuu soka Tanzania
bara iliendelea tena leo October 29, hii ikiwa ni siku moja imepita toka
tushuhudie michezo sita ikichezwa Jumatano ya October 28. Leo October
29 zimepigwa mechi mbili Tanzania Prisons ilikuwa mwenyeji wa African Sports ya Tanga katika uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Dar Es Salaam ulipigwa mchezo kati ya JKT Ruvu dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Karume.
Mechi kati ya JKT Ruvu dhidi ya Azam FC ilitajwa kuwa na mvuto zaidi ya mechi ya Tanzania Prisons dhidi ya African Sports, JKT Ruvu walikuwa wanahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutoka nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu wakati Azam FC walikuwa wanahitaji ushindi pia ili waweze kutimiza point 22 na kupata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya Yanga aliyekuwa anaongoza Ligi hiyo kutoka sare 2-2 na Mwadui FC.
Azam FC wakiwa na kocha wao muingereza Stewart Hall walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-2, magoli ya Azam FC yalifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 4 na John Bocco aliyefunga magoli mawili dakika ya 6 na kipindi cha pili akapachika goli la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 64 kabla ya Kipre Tchetche aliyetokea benchi kuja kupachika goli la nne kwa Azam FC dakika ya 90 wakati magoli ya JTK Ruvu yalifungwa na Najim Magulu dakika ya 31 na Samwel Kamuntu.
Matokeo ya mechi nyingine ya Ligi Kuu iliyochezwa leo October 29- Tanzania Prisons 1 – 0 African Sports
Post a Comment