Safari ya Mgombea Urais kupitia CHADEMA na Umoja wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa kujitambulisha Mikoani na pia kutafuta Wadhamini yeye pamoja na Mgombea Mwenza Juma Haji Duni imeendelea kwa siku nne Tanzania.
Safari ilianzia Mbeya August 14 2015, siku iliyofuatia ilikuwa Arusha, alafu ikaendelea Mwanza na August 17 2015 ni zamu ya Zanzibar.
Ninazo pichaz nyingine toka Mwanza kama haukufikiwa nazo zote unaweza kupitia hapa kuona ilivyokuwa hiyo jana August 16 2015.
Watu wa Mwanza waliokusanyika katika Viwanja vya Furahisha kumpokea Mgombea huyo wa Urais.
Lawrence Masha, aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge miaka ya nyuma, alitangaza kujiunga CHADEMA kutokea CCM… Nae alitambulishwa rasmi wakati wa mapokezi ya Lowassa.
Mabango huwa hayakosi kwenye Mikutano ya Kisiasa, Mwanza walikuwa na hili pia.
Bango jingine ni hili.
Msafara ukikatisha Mitaa ya Mwanza.
Wengine ni hao na pozi la nguvu juu ya miti, hakuna anaetaka kupitwa.
Mikutano ya Siasa na Vioja vyake, hili ni sanamu limevalishwa nguo, miwani na mabango kabisa.
Freeman Mbowe aliingia hivi.
James Mbatia nae alifika hivi.
Freeman Mbowe na Edward Lowassa wakisalimiana.
Post a Comment