
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema kuwa kati ya vitu ambavyo Slaa alikuwa akivitamani basi ni Lowassa kutua rasmi CHADEMA. Aidha Mbowe alipomhoji kuhusu Urais kwani angempisha Lowassa, Slaa alikiri kuwa angebaki kuwa Katibu mkuu wa chama ili kukoleza ushindi.
Mbowe ameenda mbali zaidi na kudai kuwa familia mpya aliyoanzisha Slaa ndiyo iliyomletea maswahibu huku akitaka wana Karatu kumsamehe.
Aidha viongozi wa UKAWA leo amefanya mkutano ulioweka rekodi mpya katika viwanja vya Mbowe mjini Karatu huku mgombea Urais wa mwamvuli huo ndugu Edward Lowassa akiahidi huduma bora za afya kwa kina mama wajawazito.
Taarifa za ndani zimedai kuwa UKAWA waliahirisha mkutano wao wakimsubiri mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Magufuli kumaliza kwanza kupita jimboni humo baada ya uvumi kuzagaa kuwa Slaa angepanda jukwaani kumnadi Magufuli hivyo kueneza propaganda ambazo zisingeweza kujibiwa kwenye jukwaa ndani ya jimbo hilo.
Post a Comment