Social Icons

Loading...

SHTUKA...Ubunifu unahitajika kuzuia mpenzi wako au mume wako KUCHEPUKA...Soma zaidi...

love
Tukija katika mambo yetu ya chumbani zaidi, ubunifu unahitajika sana tena bora uzembee kwenye kazi unayofanya kuliko kutokuwa mbunifu kwenye eneo hilo linalohusu mapenzi ambayo yametawala dunia. 

Shoga, kila siku unatakiwa kuwa mbunifu wa mapenzi kuhakikisha mumeo anafurahi kuwa nawe mnapokuwa kwenye uwanja wa fundi seremala na mkishamaliza kufanyiana mambo yenu ya chumbani zaidi afungue droo na kutoa pochi yake kisha akupatie fungu la kutosha ukanunue chochote ulichopungukiwa. 

Kama ulikuwa huna utamaduni wa kuangua kilio wakati anakushika hapa na pale, anza kulia mwanakwetu huku ukimuita kwa majina yake yote na kumsifia kwa jinsi anavyokufurahisha. 

Shoga, kama huwa unapenda kutumia mtindo mmoja tu, hebu mbadilishie uone atakavyokusifia, kama ulikuwa hujui ni nguo gani ukivaa zinahamasisha akuhitaji hata kama alikuwa hana mpango wa kula tende zake, anza kumvalia nguo za mitego mkiwa chumbani, huo ndiyo ubunifu ninaouzungumzia. 

Kwa kifupi shoga yangu unapaswa kuwa mbunifu kila idara ili kumfanya mumeo akuwaze wewe na kutofikiria michepuko ya nje ambayo hutumia ubunifu kuwanasa waume za watu na siyo limbwata kama wengi wanavyodai kwani mapenzi ni utundu na siyo uchawi. Bye!
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top