Social Icons

Loading...

BEAKING NEWZZZ!!KASI YA WAZIRI MKUU MAJALIWA NI ZAIDI YA MAGUFULI,ADAI RIPOTI KWANINI MABASI YAENDAYO KASI HAYAJAANZA...SOMA ZAIDI...

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (pichani), ametaka apatiwe  taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dart) haujaanza kazi hadi sasa. 
 
“Kesho (leo) saa 4:00 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu Dart na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo. Je, ni lini yataanza kazi, je, ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusizihuishe ili kuondoa hivyo vikwazo,?” Alihoji Waziri Mkuu.
 
Aliongeza: “Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es Salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni Tamisemi.”
 
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dk. John Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.
 
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya Tamisemi jijini Dar es Salaam.
 
Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano. Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa Tamisemi, Katibu Mkuu wa OWM-Tamisemi, Jumanne Sagini, alimweleza baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo katika utendaji wake wa kazi. Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. 
 
Pia alisema vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.  Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top