Social Icons

Loading...

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGA TENA MAJIBU ZAIDI YA MAJIBU ALIPOULIZWA KUHUSU NDOA...SOMA HAPA UJIONEE...

Inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusu mipango ya harusi ya staa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na Zari sasa basi ameyajibu kupitia kipindi cha Mseto cha Citizen kinachoendeshwa na Willy Mtuva.
Harusi haina muda mrefu kwa sababu unajua ndoa inakuwa inapagwa na mwenyezi Mungu kwa hiyo  nisingependa kuzungumza kitu cha uongo, kwanza tulikuwa tuzae mtoto na hatukutaka kupalamiana kuoana  pasipo kujuana kiundani zaidi kwa hiyo panapomajaliwa nitatangaza rasmi ni lini masuala ya ndoa‘ – Diamond Platnumz
Willy Mtuva:Zari ni mtu maarufu nje ndani ya nyumba yukoje?
Yuko vizuri kwasababu kwanza kikubwa anajua kuna maisha ya umarufu na maisha ya kutafuta pesa na usipoweza kujiongoza mtu anaweza kutumia pesa vibaya anajua kwamba ana mwanaume ambaye anahitaji kupikiwa, anatakiwa kuandaliwa maji na vitu vingine kwa hiyo ni mwanamke anayejitambua’ – Diamond Platnumz

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top