Social Icons

Loading...

EDWARD LOWASSA,SUMAYE,MBOWE KUONGOZA MAMIA WA MWANZA KUMUAGA KAMANDA MAWAZO,SOMA UTARATIBU MZIMA HAPA...

Image result for lowassa+mbowe
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anatarajiwa kuwaongoza viongozi mbalimbali wa chama hicho, wafuasi na wakazi wa jijini la Mwanza leo kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Visiwani), Salum Mwalimu, alisema licha ya Lowassa pia viongozi wengine wakuu wa chama hicho akiwamo Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye na Mwenyekiti wa Taifa (Chadema), Freeman Mbowe, watahudhuria hafla hiyo.
 
Katika kuhakikisha mwili wa Mawazo unaagwa kwa heshima na taadhima, mheshimiwa Lowassa, Sumaye na Mbowe, watawaongoza wanachama na wafuasi wa chama hicho kutoka sehemu mbalimbali wakiwamo wabunge katika viwanja vya Furahisha jijini humu,îalisema Mwalimu.
 
Mwalimu alisema baada ya baba mdogo wa marehemu Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko na Chadema kupata ushindi mahakamani dhidi Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza ili kumuaga kwa heshima zote za kiimani na kichama jijini Mwanza, alilishukuru jeshi la polisi kwa kudai litaweka ulinzi katika shughuli nzima za kuagwa kwa mwili huo.
 
Aidha, alisema viongozi wa Chadema na kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, walikutana na kuzungumzia jinsi ya shughuli hiyo itakayofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.
Kwa kipindi chote cha wiki mbili, Chadema na wafuasi wetu tumekaa kwa amani na utulivu, hivyo lazima polisi wafahamu amani hailindwi kwa bunduki nzito nzito,îalisema.
 
Hata hivyo, alisema shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa Mawazo, ulitaka kuingia dosari baada ya mkurugenzi wa halmashauri ya Ilemela, John Wanga, kutaka kuwagomea Chadema kuagwa kwa mwili huo katika uwanja wa Furahisha kwa madai ya kuwapo na ugonjwa wa kipindupindu wilayani humo.
Tumeyamaliza baada ya leo (jana) asubuhi mkurugenzi kutupatia kibali cha kuagwa mwili wa marehemu Mawazo kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana,î alisema.
 
RATIBA
Mwalimu alisema ratiba ya shughuli za kuagwa kwa mwili huo leo zitaanzia hospitali ya Rufaa Bugando saa 2:00 asubuhi hadi saa 3, wakati mwili huo utakapopelekwa nyumbani kwa baba yake mdogo, Sweya-Nyegezi kwa ajili ya ibada na ndugu, majira kuaga.
 
Alisema baada ya kutoka nyumbani kwa baba mdogo, mwili huo utafikishwa uwanja wa Furahisha kwa ibada, kuagwa na salamu za rambirambi hadi saa 8, mwili huo utakaposafirishwa kuelekea mkoani Geita.
 
Mwili ukifika Geita utahifadhiwa katika hospitali ya mkoa, kisha utaagwa Jumapili katika uwanja wa Magereza kabla ya jioni kupelekwa Katoro jimbo la Busanda ambako aliwania ubunge na hatimaye kijijini kwao Chikobe, ambako Jumatatu atazikwa,î alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Hata hivyo, alitoa rai kwa wafuasi wa chama hicho kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwapo.
 
Marehemu Mawazo aliuawa kikatili kwa kupigwa na mapanga na shoka Novemba 14, mwaka huu, katika kijiji cha Katoro na watu wasiojulikana akiwa amepakizwa kwenye ‘bodaboda’...

==>ippmedia

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top