Social Icons

Loading...

JE UNASUMBULIWA NA NGUVU ZA KIUMEE AU MWENZI WAKO ANA TATIZO HILO SOMA HAPA UPATE TIBA...




Tatizo hili kwa kawaida huwapata watu wenye umri mkubwa hasa kuanzia umri wa miaka sitini na wagonjwa wenye magonjwa sugu kama shinikizo la damu, kisukari, kansa, kifua kikuu, ukimwi na wale wanaotumia madawa kwa muda mrefu. Mfano baadhi ya dawa za shinikizo la damu, moyo, kansa, vidonda vya tumbo na nyingine nyingi ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kisayansi hasa baadhi ya dawa za asili huweza kukuathiri kabisa badala ya kukusaidia.Upungufu wa nguvu za kiume kwa sasa huwapata watu wa rika zote hasa vijana na watu wazima, kwa wazee tatizo la nguvu za kiume kupungua ni kawaida. Ieleweke kwamba kwa mwanaume kadiri umri unavyosonga mbele, uwezo wa kufanya tendo la ndoa unapungua taratibu kama una afya njema, lakini kama hali hiyo imekutokea katika umri mdogo wa chini ya miaka 35, basi ujue una tatizo linalohitaji ufanyiwe uchunguzi hospitali na siyo mahala pengine. CHANZO CHA TATIZOTatizo la upungufu wa nguvu zakiume limegawanyika katika sehemu kuu tatu kutegemea na chanzo halisi na mtu mwenyewe, vyanzo vyake havilingani. Tatizo linagawanyika kama ifuatavyo:Tatizo la kisaikolojia. Hii ni hali inayoweza kumtokea mtu yeyote awe kijana, mtu wa makamo au mzee. Hii huwa na hali mbalimbali za kimaisha hasa msongo wa mawazo, kupania kutaka kufanya tendo lenyewe, woga, wasiwasi au hofu na mazingira ya mahali pa kufanyia tendo pia yanaweza kukuathiri. Pia kutokuwa tayari na kujilazimisha kufanya tendo ni mojawapo ya sababu zinazoweza kukusababishia upate tatizo hili. Chanzo cha pili kinaitwa ‘pathological’ yaani kutokana namagonjwa ambayo tumeshayataja hapo awali mfano presha ya juu na sukari na mengineyo.Tatizo hili la magonjwa huathiri mfumo wa damu, misuli na akili kwa ujumla kwa hiyo utaona kwamba tatizo hili pia huathiri kisaikolojia. Chanzo cha tatu ni matatizo katika mfumo wa mwili. Hapa mwili unashindwa kudhibiti na kuwezesha mfumo wa mwili kufanya kazi hasa kwa upande wa nguvu za kiume. Tuelewe kwamba ili uume uwe na nguvu lazima kuwe na mfumo mzuri wa damu unaosambaa hapo ili kuinua nguvu na kukuwezesha uwe imara. Nguvu za kiume huwezeshwa na mfumo wa homoni za kiume hasa Testosterone na uwepo wa kemikali katika misuli ya uume hasa kemikali ya Nitric Oxide. Mfumo wa fiziolojia ukiathirika huvuruga pia mfumo wa homoni na hizo kemikali. Kwa hiyo ukiangalia kwa undani, upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo pana linalohitaji uchunguzi wa kina. JE, KUNA DAWA ZA KUONGEZANGUVU ZA KIUME?Hakuna dawa maalumu ya kusema kwamba hii itatumiwa na kila mtu ili kuongeza nguvu. Tatizo linatibika kutegemea na chanzo cha tatizo. Tumeona vyanzo vipo vitatu, kati ya hivyo tiba inaweza kuwa ushauri nasaha, mapumziko, kuacha kutumia dawa fulani ambayo unahisi ni chanzo au kutibu ugonjwa unaokusumbua. Asikudanganye mtu kusema ana dawa ya kutibu upungufu wa nguvu za kiume, dawa nyingihuongeza nguvu kwa muda, ili upone ni vema ufanyiwe uchunguzi wa kina ili kujua chanzo ni kipi kati ya hivyo vitatu. Baada ya chanzo kujulikana unaweza kutibiwa na kupona kuliko kutumia tu dawa bila ya ushauri wa daktari hospitali. DALILI ZA UGONJWADalili kuu ni uume kutosimama vizuri au kutosimama kabisa pale unapohitaji kufanya tendo. Nyingine ni uume kulegea na kushindwa kuendelea. Hali hii inapotokea mwili wote hunyong’onyea na kubaki katikahali ya wasiwasi na kukata tamaa.Ukifikia katika hali hii, hamu ya tendo la ndoa hupotea kabisa na unaweza kukaa muda mrefu bila kuhitaji kufanya tendo kiasi kwamba inaweza kukuletea ugomvi katika mahusiano yako.ATHARI ZA TATIZOUpungufu wa nguvu za kiume kwa muda mrefu inaweza kukufanya upate tatizo la kuwahi kumaliza tendo la ndoa au kufikia mshindo mapema chini ya dakika tatu yaani ukawaunamudu tendo kwa dakika moja hadi mbili hali iitwayo kitaalamu ‘Premature ejaculation’. Tatizo hili pia huleta tatizo katika mahusiano na kuathiri kisaikolojia na kushindwa kabisa kufanya tendo. Premature ejaculation huwa inatibika na ukarudi katika hali ya kawaida. Tatizo hili tutakuja kulizungumzia katika makala zijazo.Athari nyingine ni kupoteza uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa muda hadi unapochunguzwa na kutibiwa.Hali hii inaitwa kitaalamu ‘impotence’ au ukhanithi. Mtu mwenye tatizo hili akishagundulika chanzo ninikatika hivyo vitatu, ndipo anapewa dawa za hospitali za kuongeza nguvu kama Viagra na nyinginezo. UCHUNGUZI NA TIBAUchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa kwa madaktari bingwa kwa kuzingatia hivyo vyanzo vitatu.Daktari atakufanyia vipimo mbalimbali kama vya damu baada ya historia ya kina ya tatizo lako kueleweka. Matibabuyatategemea na uchunguzi. Wahi hospitali kwa uchunguzi wa kina, epuka kutumia dawa zinazotangazwa tu bila ya kufanyiwa uchunguzi hospitali.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top