Katikati ya Jiji la Dar es Salaam hili zoezi lilianza muda mrefu zaidi ya mwaka sasahivi, ambapo ilipigwa marufuku kabisa madereva wa bodaboda na Bajaji kuonekana wakisafirisha wateja wao kuingia katikati ya Jiji, headlines leo zinaigusa Nairobi Kenya !! Bodaboda marufuku katikati ya Jiji.
Hiyo stori imeripotiwa na Kituo cha TV cha K24 ambapo madereva wa bodaboda wenyewe wameonekana kulalamikia agizo hilo wakisema kwamba wanazuiwa kuingia katikati ya Jiji lakini hawajaoneshwa wapi ni eneo rasmi haswa ambapo wanatakiwa kufanya shughuli zao.
Kingine ambacho kimetengazwa Nairobi ni kwamba mkikamatwa mnakatisha katikati ya Nairobi, abiria pamoja na dereva wote mnapigwa faini… stori iko kwenye hii video pia.
==>Millardayo.com
Post a Comment