Social Icons

Loading...

KIPINDU PINDU CHAHATARISHA MAISHA YA WANANCHI HUKO SINGIDA...PATA MAELEZO NA PICHA MBALIMBALI KUHUSU KIPINDU PINDU SINGIDA...

RMO
Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida Dkt. Ernest Mgeta akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya ugonjwa wa kipindupindu Mkoani humo ambapo hadi sasa watu 23 wamefariki dunia.
NYAMBI
Mfanyabiashara maarufu wa soko kuu la Maniapss ya Singida, Robert Anyambilile akizungumza na waandishi wa habari sokoni hapo juu ya hali ya ugonjwa wa kipindupindu huku akiwataka wananchi kuhakikisha kuwa ufasi wa mazingira kwa kila eneo unazingatiwa katika soko hilo ili kuepukana na hatari ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu.
RAS
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida (RAS) Festo Kang’ombe akizungumza juu ya kipindupindu mkoani singida.
MATUNDA
Baadhi ya wauzaji wa matunda kituo cha stendi ya zamani wakiuza matunda yao.
WAUZAJI
Mmoja wa wafanyabiashara wa matunda katika soko kuu la Manispaa ya Singida akiuza matunda yake bila kujali kanuni za usafi wa mazingira.
AFISA AFYA
Afisa afya wa Mkoa wa Singida Joseline Ishengoma akizungumza katika hospitali ya Mkoa wa Singida .(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
JUMLA ya watu 23 wamefariki dunia huku 48 wakithibitika kuugua ugonjwa hatari wa kipindupindu kuanzi mwezi Septemba mwaka huu hadi sasa Mkoani Singida.
Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa huo (RMO)Dkt Ernest Mgeta wakati akizungumza na waandishi wa habari  juu ya hali ya ugonjwa huo ulivyo sasa.
Dkt, Mgeta alisema kuwa katika kipindi hicho jumla ya watu 1,300 waliripotiwa kuwa na ugonjwa wa kuharisha  na kutapika lakini baada ya vipimo ilibainika kuwa wenye virusi vya ugonjwa wa kipindupindu ni 48 tu.
Aidha alisema kuwa baada ya kubainika kuwepo kwa ugonjwa huo, Mkoa umeweka kambi mbalimbali katika maeneo ambayo yameonekana kuathirika zaidi na ugonjwa huo ambapo hadi sasa kuna juma ya kambi 15.
Alisema hivi sasa kuna makambi katika maeneo ya Sefunga, Singida vijijini, Mkalama, Ikungi na Manispaa ya Singida ambazo ndizo Wilaya zinazoonesha kuwepo kwa ugonjwa huo, huku Wilaya ya Iramba na Manyoni hakuna mgonjwa wa kipindupindu  hadi sasa.
“Wilaya ya Singida vijijini ndio wameathirika zaidi kwani hadi sasa watu 21 wamefariki dunia huku Wilaya ya Mkalama waliofariki dunia  ni wawili, hii inamaanisha kuwa tahadhari zaidi zinahitajika katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kuhimiza usafi wa mazingira kwa kila eneo.” Alisema Dkt, Mgeta.
Hata hivyo Dkt, Mgeta alisema kuwa hivi sasa Mkoa umegawa kwa wadau vibuyu mchirizi 4,600 ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kuhakikisha kuwa kila kaya inakuwa na choo bora.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Festo Kang’ombe alisema  hivi sasa Mkoa wa Singida umeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kila kaya inafanya usafi na kupiga marufuku uuzaji holela wa vyakula na matunda katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo mila potofu ya baba Mkwe kutokutumia choo kimoja na wakwe zake lakini wanakabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha kuwa gonjwa hilo linaondoka Mkoani Singida.
Hata hivyo Katibu Tawala huyo wa Mkoa amepiga marufuku mikusanyiko na minada yote ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kupambana na ugonjwa huo ambao chanzo chake kikuu ni uchafu.
==> Jamiiyetubongo.com

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top