Social Icons

Loading...

KIVUMBI CHA MAPENZI: RICKY ROSE KUVUNJA UCHUMBA NA MPENZI WAKE LIRA GALORE...SOMA HAPA KISA KAMILI...

CEO wa lebo ya Maybach Music Group (MMG) Rick Ross ameingia kwenye headlines za burudani baada ya mtandao wa TMZ Marekani kuripoti kuwa mapenzi na mahaba kati ya rapper huyo na mchumba wake Lira Galore yapo matatani kuisha!
Imepita miezi miwili tu toka Rick Ross aweke headlines nyingi sana kwenye social networks na websites baada ya kutangaza kuwa amemvesha pete ya uchumba mpenzi wake Lira Galore na very soon wawili hao watakula kiapo cha kuishi milele kama wanandoa… hali leo ipoje?!
ROSSAY2
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wawili hao wameingia kwenye majibishano makubwa kitendo kilichopelekea Lira kuamua kupaki vitu vyake na kuhama kwenye nyumba ya Rick Ross, japo chanzo cha ugomvi wao bado hakijaweka hadharani ila Rossay ameonekana kukubaliana na kitendo hicho na kusita kuongea kitu chochote kwa sasa huku baadhi ya mitandao Marekani ikiripoti kuwa kuvunjwa kwa engagement hiyo ni kutokana na Lira kukutwa na mtu mwengine!
ROSSAY3
Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa, Rick Ross alifanya maamuzi ya kumvesha mpenzi wake pete ya uchumba yenye thamani zaidi ya milion 700 za Kitanzania katikati ya mwezi September mwaka 2015 baada ya wawili hao kuchagua pete hiyo kwenye duka la pete jijini New York.
ROSSAY2
Pete ya uchumba aliyovalishwa Lira Galore na Rick Ross.
Lakini kabla ya kutengana dada huyo alipata shavu la kuonekana kwenye video mpya ya Rick Ross ” Sorry Video” na pia kuonekana na rapper huyo kwenye tuzo za BET Hip-Hop Awards mwezi mmoja uliopita, isitohe mwaka 2012 Lira alishawahi kujitabiria kupitia page yake ya Twitter kuwa atakuja kufunga pingu za maisha na rapper huyo lakini kwa muonekano wa mambo sasa hivi inaonekana kama ndoto hizo zinaweza kuishia njiani.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top