Kumekuwepo na sintofahamu juu ya hatma ya kuuzika mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Geita Alponce Mawazo baada ya kutokea kwa mvutano kati ya UKAWA na Jeshi la Polisi.
UKAWA pamoja na ndugu wa marehemu jana waliamua kufungua kesi katika mahakama kuu ya Mwanza wakipinga kauli ya RPC wa Mwanza Charles Mkumbo aliyoagiza kusiwepo shughuli za kuaga mwili wa marehemu huyo kutokana na kuwepo Ugonjwa wa Kipindupindu kilichoibuka maeneo mbalimbali ikiwemo ndani ya Mwanza yenyewe.
Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallyawalifika Mahakama Kuu Mwanza na kesi tayari imesomwa.
Leo mahakama kuu Mwanza imetoa maamuzi ya kusikilizwa kwa maombi ya familia ya marehemu Mawazo kuhusu ndugu yao kuweza kuagwa na kufuatwa kwa taratibu zote za mazishi, kwa sasa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.
Post a Comment