Uchaguzi Mkuu Tanzania umekwisha na zile headlines mfululizo kuhusu Siasa zimeanza kupungua pia, lakini hazijaisha… YES !! Bado headlines zitaendelea kutufikia kwa sababu kuna Majimbo ambayo Uchaguzi ulisogezwa mbele baada ya kutokea matatizo mbalimbali ikiwemo Wagombea wake kufariki.
RIP Marehemu Deo Haule Filikunjombe… stori inagusa Jimbo lake sasahivi, ni Jimbo la Ludewa lililopo Mkoa wa Njombe.
Mchakato kwenye Jimbo hilo umeanza, kwa upande wa CCM ndio kumeshika kasi yenyewe, kwenye majina ya waliotangaza kuitaka nafasi ya Uwakilishi wa Ludewa ndani ya Jengo la Bunge Dodoma, yuko pia mchekeshaji Emmanuel Mgaya a.k.a ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi.
Hii ndio sababu ya yeye kugombea Jimbo la Ludewa >>> “Kwanza nina uhakika mimi ndio Mgombea pekee mwenye uwezo wa kuleta maendeleo… nilikuwa na wazo la kugombea Ubunge lakini nilijipa muda kwanza“- Masanja Mkandamizaji.
Kwanini kagombea kupitia CCM na sio chama kingine >>> “Mimi ni mwanachama wa CCM na nimeamua kugombea nafasi hii kwa kupitia chama changu, nipo katika siasa tangu siku nyingi ingawa mwanzo sikujitokeza kwa sababu aliyekuwepo alijitosheleza.. nilichukua kadi ya Uanachama wa CCM tangu mwaka 2005.”- Masanja.
Ikitokea hajapita kwenye Ubunge Je? >>> “Nisipopita kugombea Ubunge wa Ludewa, nitampa support yule ambaye atapewa nafasi kugombea“
Orijino Komedi na Ubunge? Hapo vipi mtu wangu ? >>> “Orijino Komedi ipo, mimi sio member wa kundi… mimi ni Mwanzilishi, haimaanishi kwamba nitafanya kazi za Ubunge kwa saa 24 kila siku… maendeleo yatakuja Ludewa lakini Alhamisi kama kawaida, ‘chakachuwa nichakachuweee’… siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi.. nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…“
Wanaojiuliza kama atavaa viatu vya marehemu je? >>> “Naamini ndani ya utawala wangu jimbo la Ludewa litakuwa Jimbo la mfano, kuna wengi wanasema kama nitavaa viatu vya marehemu…! Mimi sijaja kuvaa viatu vya marehemu, ila nitahakikisha maendeleo ya Ludewa yanakua kwa kasi.”-Hivyo ndio alivyomaliza Mchekeshaji anayewakilisha kundi laOrijino Komedi, Masanja Mkandamizaji na headlines zake kwenye Ubunge waLudewa.
Post a Comment