
Yadaiwa
huenda ni kutokana na chuki za kisiasa zilizosababisha kifo cha kiongozi wa
Chadema
Geita. Mtu
ambaye hajafahamika jina wala makazi, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu
katika Kituo cha Afya Katoro wilayani Geita, baada ya kufikishwa na polisi
akiwa hajitambui.
Mtu huyo
anasadikika kupigwa na watu wasiojulikana Jumamosi saa mbili usiku, huku tukio
hilo likihusishwa na chuki za kisiasa zinazohusiana na vurugu zilizosababisha
kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Mganga
Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Daniel Izengo alisema saa 2:30 usiku walimpokea mtu
huyo aliyefikishwa na polisi akiwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani.
Awali,
mganga huyo alisema watu wawili walijeruhiwa katika vurugu zilizosababisha kifo
cha Mawazo ambao walifikishwa kwenye kituo hicho wakatibiwa na kuruhusiwa.
Pia alisema
watu watatu walifikishwa kituoni hapo juzi akiwamo Mawazo, Elizabeth Paschal
(48) na Bahati Michael (38) wote wakiwa wakazi wa Katoro.
Dk Izengo
alisema hali ya Mawazo ilibadilika na kumwandikia rufaa kwenda Hospitali ya
Wilaya ya Geita ambako alifariki dunia, huku majeruhi wengine wakipatiwa
matibabu na kuruhusiwa baada ya hali zao kuridhisha.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Geita, Lotson Mponjoli alisema upelelezi wa tukio hilo
unaendelea, ikiwamo kuwatafuta watuhumiwa.
Hilo ni
tukio la pili ndani ya siku chache, la kwanza likiwa la kifo cha Mawazo.
Chanzo:Jamiiyetubongo.com
Post a Comment