Maisha ni hatua mtu wangu ukiwa huu ni mwanzo wa mwezi November naomba nikukumbushie historia halisi ya mchezaji wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Luis Suarez ambao wengi wetu tumekuwa tukimfahamu uwanjani na sehemu kidogo ya maisha yake ya sasa.
Luis Suarez alizaliwa Salto Uguguay katika familia ya watoto saba na yeye alikuwa mtoto wa nne katika familia, kaka yake Paolo Suárez ni mchezaji wa mpira wa miguu kama alivyo yeye ila kaka yake anakipiga katika klabu ya Comunicaciones ya Guatemala. Baba na mama yake Luis Suarez walitengana akiwa na umri wa miaka tisa.
Mshambuliaji huyo akiwa na umri mdogo bado yeye na familia yake walihamia Montevideo sehemu ambayo Suarez alianza kupambana kucheza soka lakini kutokana na umasikini wa familia yake ilimlazimu awe anafanya kazi ya ufagiaji wa mitaani wa mitaani ili kujikimu kimaisha.
Luis Suarez alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Sofia Balbi toka akiwa na umri wa miaka 15 wakati yupo Montevideo, familia ya Sofia ilihamia Barcelona mwaka 2003 na Suarez kubaki Montevideo akiendelea kutafuta njia za kufanikiwa katika soka sambamba kutimiza ndoto yake ya kwenda ulaya kumfuata mpenzi wake Sofia Balbi ndoto ambayo ameitimiza.
Post a Comment