Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohmaed Shein bado ataendelea kuwa rais wa Zanzibar pamoja kuwa muda wake wa uongozi unakwisha jumatatu kwa vile hakuna rais mpya aliyeapishwa.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili ambaye ndio msemaji wa serikali Mhe Mohamed Aboud wakati akitoa taarifa ya serikali ambapo amesema kwa mujibu wa katiba kifungu cha 28 1 A kikieleza waziwazi kuwa rais aliyeko madarakani ataendelea kuwa rais hadi pale atapoapishwa mwengine.
Akizungumzia suala la uchaguzi wazanzibar uliofutwa waziri Aboud amesema serikali inakubaliana na uamuzi huo kwa vile umechukuliwa kwa muijbu wa katiba na sheria.
Katika hatua nyengine kamishna mkuu wa jeshi la polisi kamishnei ya Zanzibar CP Hamdan Omar Makame akatoa taarifa yake kwa wananchi amewaonya wale wote ambao wana mpango wa kuhatarisha amani na kuvunja sheria waachane na kitendo hicho kwa vile jeshi la polisi limejipanga kwa nguvu zote kukabilaina na tukio lolote la fujo.
Mji wa Zanzibar unaendelea kuwa na utulivu na wakazi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida huku wakiendelea kutafakari na hali ya kisiasa baada ya kuwepo taraifa mbalimbali za uchaguzi mkuu ambao matokeo yake yamefutwa na tume ya uchaguzi.
Post a Comment