Habari wakuu
Magufuli: Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
WIZARA
Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo
Mazingira: Makamba, naibu Makamba
Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
Ulemavu: Mavunde
Kilimo, mifugo na uvuvi: Mwigulu Lameck Nchemba, Nashe naibu
Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu
Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe
Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nmemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan
Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi
Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
Utalii: Waziri bado
Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
Sayansi na ufundi: Naibu ni Stella Manyanya
Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
Habari: Nape Nnauye
Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene
Swali: Tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua?
Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata
Umesema kukutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?
Niliyowachagua wote wana CCM na walinadi ya sera hapa kazi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.
Manyerere Jackton: Kwa kupunguza baraza la mawaziri, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?
Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34.
==>http://habari-zetutz.blogspot.com/
Post a Comment