Social Icons

Loading...

BREAKING NEWZZZ!!! KASI YA MAGUFULI YATINGA MSKITINI,MUFTI WA TANZANIA AMSAMISHA KAZI MAJALIWA KWA KASHFA YA MAGARI 82...SOMA ZAIDI...



MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakari Zuberi amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Utawala wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Karim Majaliwa kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya kashfa ya magari 82 pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Mufti alisema anatumia mamlaka aliyonayo kumsimamisha mkurugenzi huyo. Hivi karibuni, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iliijia juu Bakwata na kuitaka itoe maelezo ya ongezeko la maombi ya msamaha wa kodi katika utoaji wa magari yanayopitishwa katika taasisi hiyo ya dini, kutoka nje ya nchi.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, taasisi hiyo ya dini imekuwa na ongezeko kubwa la maombi ya msamaha wa kodi kwa magari ya nje ambapo tangu mwaka 2006 hadi Septemba mwaka huu, imeingiza magari 82 ya aina tofauti.
Katika barua ya TRA kwa taasisi hiyo iliyosainiwa na Meneja Misamaha ya Kodi, Mwantumu Salim ya Novemba 19, mwaka huu, ilibainisha kuwa kutokana na idadi kubwa ya magari ya msamaha pamoja na maombi kuzidi kuongezeka, mamlaka hiyo imeamua kuichunguza taasisi hiyo ili kujua magari hayo yanavyotumika.
Aidha, TRA ilitoa siku saba kwa Bakwata iwasilishe kadi za usajili wa magari, kitabu kinachoonesha safari za magari, stakabadhi za kulipia mafuta, bima, huduma za matengenezo ya magari ikiwemo ushahidi wa maelezo na ushahidi kuhusu fedha zilizotumika kununua magari hayo pamoja na hesabu za mwaka za taasisi.
TRA ilifikia hatua hiyo baada ya Bakwata kuwasilisha maombi ya msamaha wa kodi kwa TRA kwa ajili ya kuingiza nchini gari aina ya IVECO ambao hata hivyo msamaha huo ulikataliwa hadi uchunguzi huo utakapokamilika.

==>duniayakotz.blogspot.com
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top