Social Icons

Loading...

MBUNGE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR,ASEMA NI KUCHOCHEA MGOGORO UCHAGUZI MKUU WA OCTOBER 2015,SOMA ZAIDI...

Mbunge wa Jimbo la Malindi Zanzibar, Ali Saleh, amesema kufanyika uchaguzi wa marudio kabla ya kupatikana maridhiano, ni sawa na kuchochea mgogoro wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
 
Saleh amesema iwapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda viti vyote vya majimbo ya uwakilishi 54 Unguja na Pemba, kitakwama kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kuibua mgogoro mpya wa Katiba utakaoitingisha Zanzibar.
 
Akizungumza na Nipashe mjini Unguja jana, alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), inapaswa kusimamisha uchaguzi wa marudio ili kutoa nafasi ya kufanyika mazungumzo ya kusaka muafaka kutokana na mkwamo wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana.
 
Saleh alisema vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo, havina ubavu wa kufikia masharti ya Katiba ya kuunda serikali ya pamoja huku CCM ikiwa haina uwezo wa kuunda serikali peke yao kwa mujibu wa kifungu cha 42(2) cha Katiba ya Zanzibar.
 
"Ndani ya kipindi cha siku 18 baada ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais, kwa kushauriana na Makamu wote wawili Rais, atateua mawaziri kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuzingatia uwiano wa viti vya majimbo kwa vyama vya siasa vilivyomo ndani ya Baraza la Wawakilishi," alifafanua.
 
Alisema vyama vinavyoshiriki uchaguzi wa marudio havijawahi kufikisha asilimia 10 ya matokeo ya urais, jimbo au kupata kiti kimoja cha diwani tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
 
Alikitaja kifungu cha 39(i) cha Katiba ya Zazibar pia kimeleeza wazi iwapo chama kilichoshika nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia 10 ya kura zote za uchaguzi wa Rais kitatoa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
 
Hata hivyo, alisema kama chama kilichoshika nafasi ya pili kitashindwa kufikisha asilimia 10 ya matokeo ya urais, nafasi ya Makamu wa Kwanza itapewa chama chochote kilichotokea nafasi ya pili kwa wingi wa viti vya majimbo katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 
“Uwezekano wa vyama vilivyobakia katika uchaguzi kupata asilimia 10 ya matokeo au viti vya majimbo, inabakia kuwa ndoto katika uchaguzi wa marudio mwaka huu,’ alisisitiza Saleh.
 
Alisema lazima kuwe na uchaguzi wa maridhiano pamoja na tume huru inayokubalika na wadau wa uchaguzi baada ya wananchi kupoteza imani na Zec chini ya Mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top