Social Icons

Loading...

KILICHOIPONZA SIMBA FA CUP HIKI HAPA,SOMA ZAIDI,VIONGOZI WANENA MAZITO....

Baada ya michezo mitatu ya Kombe la FA kuchezwa na kushuhudia timu za Dar es Salaam Young AfricansMwadui FC na Azam FC kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, April 11 2016 ilikuwa zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga.
Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Coastal Union kutokana na timu hiyo kuaminika kuwa chini ya kiwango naSimba kuutawala mchezo, wamekubali kipigo cha goli 2-1 wakiwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
DSC_0041
Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 20 naYoussouf Sabo aliyefunga kwa mpira wa faulo. Simba walifanya mabadiliko na kumuingiza Hamis Kiiza ambaye alifunga goli la kusawazisha dakika ya 50 na kuufanya mchezo kuwa sare hadi dakika ya 85 Youssouf Sabo akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyotokana na makosa na Novat Lufungo kumchezea faulo Shiboli.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright 2025 MAWINGUBONGO | Designed By Code Nirvana
Back To Top