Social Icons

Loading...

HIZI NDIZO SABABU ZA NDANI KWA ANNA KILANGO KUFUKUZWA UKUU WA MKOA WA SHINYANGA,SOMA ZAIDI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  mamaAnna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa  sana na hali hiyo.

Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.

Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
 
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..

==>HABARIKALI1

SHAMBA LA SUMAYE LAMILIKIWA RASMI NA WAVAMIZI,SUMAYE ASEMA SHAMBA NI LAKE NA LITAENDELEA KUWA LAKE TU...SOMA HAPA...


HATIMAYE wavamizi shamba la ekari 33 la aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, eneo la Mji Mpya, Mabwepande, nje kidogo ya Dar es Salaam, wamejimilikisha rasmi kwa kuweka tangazo linaloelekeza matumizi ya shamba hilo.
Nipashe imefanikiwa kuona tangazo hilo ambalo limeandikwa kwa maneno yenye rangi nyeusi na nyekundu yanayosomeka:
Eneo hili ni la shule, zahanati, eneo la wazi kwa ajili ya wananchi wa Kinondoni ni marufuku kujenga eneo hili asanteni-Wananchi.
Baada ya Nipashe kuona tangazo hilo iliwasiliana na Sumaye juzi ambaye alikiri kufahamu uwapo wa tangazo hilo katika shamba lake na kusema halijawekwa na mamlaka bali wavamizi na kwamba ameanza kuchukua hatua mbalimbali.
“Shamba hili ni mali yangu kwa nini nilisuse, hawa walioweka tangazo kwenye shamba langu ni wavamizi sio mamlaka za serikali, watambue shamba hili ni langu na hatua mbalimbali nimeanza kuchukua, litaendelea kuwa langu,” alisema Sumaye aliyeongoza serikali 1995-2005.
Mwezi Februari, Sumaye aliliambia Nipashe kuwa maamuzi ya shamba lake yapo mikononi mwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Sumaye alitoa kauli hiyo baada ya mwishoni mwa mwezi Januari Makonda kuitisha mkutano Mji Mpya ambapo Sumaye aliutumia kwa kuonyesha wavamizi hao hati za umiliki wa ardhi hiyo yenye ukubwa wa heka 33.
Katika mkutano huo, Makonda aliomba apewe wiki mbili ili kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kupitiwa sheria za umiliki wa ardhi hiyo kama zilikiukwa lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Aidha, makonda aliwaeleza watu waliojenga kwenye shamba hilo, endapo Sumaye atashinda kisheria kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo na hakukiuka sheria ya umiliki, mstaafu huyo angeangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao.
Aliwaeleza wavamizi hao kuwa watapata eneo endapo Sumaye atakuwa amekiuka sheria za umiliki ardhi na kwamba kinyume na hapo watamuomba awakatie sehemu ingawa itategemeana na mmiliki husika.
Katika utetezi wake siku hiyo, Sumaye alisema baada ya serikali kubadili matumizi ya ardhi, waliacha kulilima miaka mitatu iliyopita ili kujengwe Chuo Kikuu.
Uvamizi wa ardhi hiyo ulitokea mwishoni mwa mwaka jana ambapo zaidi ya watu 100 waligawana eneo hilo na wengine kujenga nyumba za kudumu za matofali na kuainisha wapi kuwe zahanati, makazi, ofisi na uwanja wa michezo.
--IPPMEDI
A

KIDAMALI AHUKUMIWA KUFA KWA KITANZI...SOMA HABARI KAMILI HAPA...




MKAZI wa kijiji cha Kidamali, Joseph Balami juzi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu kanda ya Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Stani Singaile (42) kwa makusudi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Balami alitenda kosa hilo Oktoba 15, 2011 katika kijiji cha Kidamali, Wilayani Iringa, mkoani hapa.
Akisoma hukumu hiyo kwa saa mbili, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Iringa, Mary Shangali alisema amekubaliana na ushahidi uliotolewa kwamba pasipo shaka mtuhumuwa alitenda kosa hilo.
“Kwenye kesi hii upande wa mashitaka ulileta mashihidi watano na upande wa utetezi ulileta mashahidi wawili ambao ni mtuhumiwa mwenywe na mke wake," alisema Jaji Shangali.
"Mahakama imekubaliana na upande wa mashitaka kuwa mtuhumuwa ametenda kosa na imemtia hatiani kwa kosa la kuua kwa makusudi.
"Kwa kuwa adhabu inayotolewa kwa kosa hilo ni moja kwa mjibu wa sheria... ninakuhukumu kunyongwa hadi kufa.”
Kabla ya hukumu kusomwa, wakili wa serilali Felix Chakela aliitaka mahakama kumpa adhabu kali mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo wakati.
Wakili wa utetezi, Chakela Lwezaula alisema yeye anasubiri hukumu ya mahakama.
Jaji huyo asema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 15, katika kilabu cha pombe za kienyeji.
Alisema mashahidi wa mashitaka wamethibitisha bila kuacha shaka kuwa siku hiyo mtuhumiwa alikwenda kwenye kilabu hicho kumfuata marehemu kisha kumchoma na kisu kifuani.
Alisema kitendo cha mtu kumfuata mtu na kumchoma kisu kifuani, hususani upande wa kushoto kinaonyesha alidhamiria kuua na kwamba kwa kitendo hicho, mahakama inamtia hatini kwa kosa la mauaji ya kukusudia.
Pia alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa pamoja na maoni yaliyotolewa na waungwana wa mahakama, yanakubaliana kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukuacha shaka kwa mtuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Balami anadaiwa kuwa katika kijiji cha Kidamali Wilaya ya Iringa majira ya saa moja usiku, alimuua Singaile kwa kumchoma na kisu wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.
Ilidawa mahakamani hapo kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia, lakini alikamatwa saa mbili usiku na kufikishwa kwenye ofisi ya serikali ya kijiji na baadae katika kituo cha polisi kwa hatua zaidi,
--IPPMEDI
A

JE WAJUA KILICHOSABABISHA KIFO CHA MSANII NDANDA KOSOVO,HIKI HAPA...


Msanii wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia asubuhi ya leo katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento, Ndanda alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo, maradhi yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.

Kardinali ambaye pia ni mjomba wake, amesema kuwa Ndanda alihamishiwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili siku mbili zilizopita kutoka Mwananyamala baada ya tatizo lake kushindikana kabla ya mauti kumkuta majira ya saa mbili asubuhi ya leo.

"Nilikuwa naye hospitali tangu jana, na nimekesha naye, ilipofika asubuhi hali yake ilikuwa nafuu, nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa damu, lakini muda mfupi baada ya kuondoka hospitali hapo nikapigiwa simu kuwa Ndanda amefariki, ilikuwa mida ya saa 2 asubuhi” Amesema Gento.

Gento amesema taratibu za mazishi zinasubiri mama yake arudi Dar es salaam, ndipo wataamua kama asafirishwe au azikwe huku
 
“Mama yake alikuwa amekwenda Lubumbashi, lakini sasa inabidi ageuze na ndege, akisharudi ndiyo tutajua kama tunazika au tunasafirisha…… mama yake ni dada yangu, kwahiyo Ndanda ananiita mimi mjomba”

Hadi mauti yanamkuta Ndada alikuwa akifanya shughuli za muziki kama msanii wa kujitegemea ‘Solo Artist’ pamoja na shughuli za kibiashara

PADRI FAZA EDWARD AFUNGUKA KUHUSU JOKATE,ASEMA YAFUATAYO...

IMG-20151118-WA0010-721x1024
 Baadhi ya watu waliodai kuwa wao ni waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako anaabudu Mbongo Fleva na Miss Tanzania No. 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wamesema nyota huyo hatakiwi kushiriki ibada kwa vile uhusiano wake na Mbongo Fleva, Ali Kiba upo wazi sana, sasa kanisa hilo limetoa tamko, tambaa na Amani.

Akizungumza na gazeti hili juzi kanisani hapo, padri aliyejitambulisha kwa jina moja la Edward ‘Faza Edward’ alisema wao kama kanisa wanamtambua Jokate kama muumini wao wa miaka mingi na kwamba mambo mengine hayawahusu.
“Jokate namtambua kama muumini wetu hapa ana anashiriki vizuri tu. Sisi hatuna tatizo naye. Kwanza sisi mtu yeyote anaruhusiwa kuja kusali hapa, hata kama ni Mwislam ilimradi tu afuate taratibu zetu.
“Kwa hiyo Jokate tunaye hapa kanisani na anaendelea vizuri tu. Umemuulizia na paroko, yeye muda huu ana wageni,” alisema Faza Edward.

Ali-mkiba-jokate-na-wema-2….Akiwa na Ally Kiba.
Awali waumini hao walisema kuwa, kitendo cha Jokate kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari akiwa na Kiba huku si mwanandoa wake jambo ambalo wao wanaliona si sawasawa kwa vile mrembo huyo hushiriki pia kuimba kwaya ya kanisa hilo.

Mwaka jana, gazeti dada na hili, Ijumaa liliandika habari yenye kichwa kisemacho; Waumini: Jokate anatutia aibu.
Katika habari hiyo, Jokate alidaiwa kuwakera waumini wenzake kufuatia kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho.
Pia, alilalamikiwa kwa tabia yake ya kupanda jukwani kwenye kumbi za muziki na kunengua huku yeye akiwa ni mwanakwaya wa kanisa hiyo.

Akijitetea kuhusu madai ya waumini wenzake katika habari hiyo, Jokate alisema kuwa, kanisa hilo halimzuii kuvaa nguo fupi wala kukata mauno jukwaani kama mwanamuziki kwani kazi ni kazi.
Alisema kanisani anakwenda kama kawaida na kwaya anaimba kama ‘kawa’.
Katika habari hii mpya, Jokaye alipoulizwa alisema: “Mimi sitaki mnifuatilie mambo yangu ya imani, sitaki kabisa, mnanikwaza.” 

UFISADI WA WABUNGE KWENYE KAMATI ZA BUNGE ZAFIKIA PABAYA,WAZIRI ATOA TAMKO,JE TAMKO GANI NA WAZIRI GANI...SOMA HAPA...

mtz1

Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea kuchunguza tuhuma zinazowakabili baadhi ya wabunge kwa kupokea rushwa kwenye Kamati za Bunge, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, amesema Bunge linapaswa kujisafisha.

Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Nipashe baada ya kumalizika kwa ibada ya mkesha wa Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro.

Alisema kama tuhuma za rushwa zinazoelekezwa katika Bunge zina ukweli, Bunge linapaswa kujisafisha kwa kuwa ni mojawapo wa mhimili wa serikali unaotumainiwa na wananchi.

Alisema Watanzania wana imani kubwa na wabunge katika kuwatatulia kero zao kwa kuwa wao ndiyo wawakilishi wa wananchi, hivyo tuhuma zinapowakabili wanapaswa kijisafisha na kuwa wasafi.

“Siwezi kuzungumza kwa undani zaidi kwa kuwa sote hatujui kama ni kweli au la, lakini ninachoweza kusema ni kama tuhuma hizo zina ukweli, basi Bunge linapaswa kujisafisha,” alisisitiza Mabula.

Kadhalika, amewaasa Watanzania kutenda matendo mema wakati wote.

Kumekuwapo na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wenyeviti wa Kamati za Bunge, huku wabunge wengine wakijiuzulu kwa kutaka mamlaka za kiuchunguzi wachunguze tuhuma hizo na sheria ichukue mkondo wake.

Baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kupokea rushwa ni wa Kamati ya Maendeleo na Huduma za Jamii, hali iliyosababisha wabunge 12 katika kamati hiyo kusaini waraka maalum wa kupelekwa kwa Spika kutaka kujiuzulu, huku Spika wa Bunge, Job Ndugai, akifanya mabadiliko ya wenyeviti watano wa kamati hizo.
CHANZO: NIPASHE

RAIS JPM AMPONGEZA MBUNGE NASSARI ASEMA USONI NI CHADEMA ILA MOYONI NI CCM...SOMA HAPA...


Rais Dk. John Magufuli amesema amejitolea kuwa sadaka kwa  Tanzania katika vita dhidi ya mafisadi na kwamba akishindwa kufanya hivyo, hakuna sababu ya yeye kuitwa rais.

Pia amesema wote waliotumbuliwa majipu watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumza jana katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika sehemu ya barabara ya Sakina hadi  Tengeru yenye urefu wa kilomita 14.1, itakayokuwa na njia nne, alisema ataendelea  kutumbua majipu kwa kuwa wanaonufaika na kudidimiza uchumi wa nchi ni wachache.

“Tumeanza kuchukua hatua ndogo ndogo, tunatumbua majipu. Mpaka sasa waliotumbuliwa si wengi kiasi hicho, hawajafika hata 2,000. Juzi juzi nimesikia baadhi ya watu wameanza kuwatetea wanaotumbuliwa, nasema hao wanaowatetea washindwe na walegee,” alisema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, Dk. Joseph Butore, Makamu wa Pili wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga, Balozi wa Japan nchini na mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Alisema wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida na taabu kutokana na wachache kufilisi mali na rasilimali za nchi.

“Ifike mahali mmoja lazima ajitolee kufanya kazi hii. Mimi nimeamua kuwa sadaka kwa Tanzania, lazima tufanye kazi ya kutumbua majipu na kuwaletea maendeleo wananchi.

“Nisipofanya hivyo, hakuna sababu ya mimi kuitwa Rais. Hii  nasema kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwangu, naomba Watanzania waniombee,”alisema.

Alisema kwa mfano yapo mambo ya hovyo ambayo hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeisababishia serikali upotevu wa fedha za matumizi ya simu nje ya nchi husika (roaming) kiasi cha Sh. bilioni 200.

Alisema watu wote wanaojihusisha na ufisadi watafukuzwa na kufikishwa mahakamani mwishowe kufungwa ili nao wakapate machungu.

“Hii nchi ilifika mahali ikawa kama  shamba la bibi vile,” alisema na kusisitiza kuwa katika kuwaletea wananchi maendeleo hatafanya ubaguzi wowote kwa kuzingatia vyama, dini, kabila ila atachapa kazi tu.

“Nawaomba Arusha tujenge umoja wetu, tusibaguane. Tukianza kujenga umoja wa Tanzania na tukaunganishaa na umoja wa Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini, Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na maendeleo ya kasi," alisema Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aliongeza kuwa: "Tukiamua tunaweza kubadilika na kuwaletea wananchi wa jumuiya hii maendeleo makubwa.”
 
Alisema wananchi wa EAC wanachohitaji si vyama ila kazi, maendeleo na maisha mazuri na si kuwafanya wachache wawe wanafaidi kuliko wengine.

Awali, alimpongeza Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), kwamba ni mtu mchapakazi.

“Nampongeza sana Nassari, ni kijana safi anachotaka ni kazi na ameweza kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top