Social Icons

Loading...

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA,PICHA ZOTE ZIKO HAPA...

Watanzania 13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika kituo cha polisi cha Fika salama karibu na Mto Katonga wilaya ya Mpigi huko Kampala, Uganda.

Ajali hiyo imehusisha  gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia watu hao wakiwemo watanzania ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye  harusi ya binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Nkozi pamoja na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi nchini humo.
 
Source: Mpekuzihuru.

MBUNGE LIVINGSTONE AAPA KUPAMBANA NA WATUMISHI WAUZA UNGA...JE AKNANI HAO SOMA HAPA...




MBUNGE wa Mtera mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde (CCM), ameapa kutowaonea haya watumishi watakaobainika kuhusika na wizi wa dawa katika vituo vya kutolewa huduma jimboni mwake.Lusinde, maarufu kama Kibajaji, aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Nipashe, juu ya mikakati ya kuboresha huduma za afya, ikiwamo upatikanaji wa dawa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo.
Alisema katika hatua za awali, atahakikisha kiasi cha dawa kinachopelekwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika zahanati na vituo vya afya, kinaongezwa ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la watu.
“Tutanza na kuongeza idadi ya dawa kwani hivi sasa hatuwezi kusema moja kwa moja kuwa kuna wezi kwani idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kila kukicha, lakini kiasi cha dawa hakiongezeki, hivyo kusababisha watu wengi kukosa dawa,” alisema.
Alisema baada ya kuongeza kiwango cha dawa, kazi itakayofuata ni kusimamia utoaji na usambazaji ili kuangalia kama kuna wizi unafanyika au la.
Lusinde aliongeza kuwa kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), watasimamia vituo ambavyo vimekuwa vikitoa huduma chini ya kiwango, hivyo kusababisha watu kukimbilia zahanati ambazo zimekuwa na unafuu.
“Tutawasimamia watumishi ambao wamekuwa hawafanyi kazi zao kwa ufanisi na kusababisha foleni ndefu za wagonja katika zahanati moja kwa madai kuwa ndiyo inayotoa huduma nzuri zaidi ya zingine,” alisema.
Pia alisema atahakikisha watumishi ambao wamekuwa wakicheleweshewa mishahara yao wanapewa kwa wakati ili kuwaongezea ari katika kufanya kazi.
==>IPPMEDIA

JE NI KWANINI WANAWAKE WENGI WAREMBO HUISHIA KUWA MICHEPUKO???HAYA MAJIBU HAPA SOMA ZAIDI...

Ni ukweli kwamba wako wanawake wengi sana ambao wanahesabu kuwa ni baraka na jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwaumba wenye sura nzuri na wenye mvuto. Pamoja na ukweli huu, ni wazi na imethibitika kwamba wako wanawake ambao wanahesabu kuzaliwa warembo ni mojawapo ya laana au mkosi kwasababu ya zile hali ambazo wamezipitia hususani katika mahusiano yao ya kila siku na wanaume.

Mara kwa mara kumekuwepo na tabia ya wanaume kutamani sana kuwa kwenye mahusiano na wanawake warembo, na hupenda kuwatongoza hao mara kwa mara ingawa moyoni mwao wanawaangalia warembo hawa kama wasichana wa kula nao raha tu “good time girls” na wala sio wake wakuoa.

Utakubaliana na mimi labda umewahi kuona mwanaume anakuwa kwenye mahusiano na binti mzuri sana kisura na kiumbo tena wanakuwa kwenye mapenzi kwa muda mrefu tu huku huyu binti akijua mbeleni kuna ndoa, ghafla ukija kusikia huyu kaka anaona unapigwa mshangao kuona wala sio yule binti mrembo anayeolewa.

Hii imewaacha mabinti wa aina hii katika maumivu makali sana ya moyo, na wengine wamekata tama na kuamua kujirahisisha ili mraadi maisha yaende. Wengine wameamua kukaa wakitunzwa na waume za watu kwasababu wao wamejithibitishia kwamba kuolewa hakupo.Tafiti zinaonyesha kwamba ukiona mwanaume aliyeamua kukaa muda mrefu na mwanamke mrembo, mara ningi unakuta ni wale wanaume wenye tabia za kisanii “players” ambao hata wao huwatumia mabinti hawa na kuwatelekeza hapo baadae.

Inasemekana imani au mtazamo huu hauko tu kwa wanaume bali hata wanawake wale wenye uzuri au urembo wa kati au wasio warembo kabisa wanajua na kuamini hivyo na mara nyingine huwarushia vijembe wale wanawake warembo kuwa “utachezewa tu na utaachwa na wataolewa wengine”. Na pale inapotokea kwenye mahusiano binti wa kawaida akagundua mpenzi wake wa kiume ametembea au husiana kinyemela na binti mrembo zaidi kuliko yeye, utakuta wakikutana kwenye kupashana au hata kwenye ugomvi wa kuandikiana ujumbe wa maneo, huyu binti wa kawaida humwambia yule mrembo kwamba “we jifurahishe tu ila usiamini kwamba utaolewa, huyu mwenzako anakuchezea tu anajuwa nani wa kuoa”. Unadhani imani hii wameitoa wapi?

Wakati mfumo au mtazamo huu unapoenea au kujirudia zaidi, wanawake hawa warembo au wazuri wa sura na umbo huamini kwamba wanaume wote ndivyo walivyo, wanaamini kwamba wanaume wote huwasogelea ili kujifurahisha kimapenzi tu na baada ya hapo kuwakimbia. Wakati huu wa kusubiria kumpata mwanaume wa kuoa “Mr. Right” ukizidi wanawake hawa huchoka na kukata tama, na hivyo wao sasa huamua kukimbizana na kutafuta mwanaume wa kuwapenda na kutulizana nao.

Tabia hii ya kuwafukuzia wanaume kwa bahati mbaya kuwagharimu sana wanawake hawa kwasababu wanaume wengi wanamtazamo hasi kwa wanawake wa jinsi hii. Wanaume wengi wanaamini wao ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kumtongoza mwanamke na sio mwanamke kuwa wa kwanza kuwatongoza wao, na mbaya zaidi anapokuwa mwanamke mzuri ndio shida huongezeka, wengine wakianza kuambiana “huyu lazima atakuwa mgonjwa anataka kuambukiza wengine”. Hapa unaweza kuelewa ni kwa kiasi gani hali huwa ya kutatiza.

Kwa upande mwingine, wanawake hawa wanaoonekana wazuri wa umbo na sura, sio halisi kama wanavyoonekana. Kwa mbali ni kweli mwanaume yeyote atavutiwa nao lakini jinsi unavyowakaribia na kuwafahamu unagundua mengi yanayohuzunisha na kuogopesha kuishi nao. Unagundua kuwa uzuri mwingine umeongezewa kutoka madukani zaidi na sio ulio halisi. Mara nyingine uzuri huu na ile hali ya kuonekana ni wagharama sana huwaogopesha wanaume wasio na kipato kikubwa na kwahiyo wanaume hawa wakishapata kabahati ka kufaidi penzi mara moja au mbili wanakimbia tena kwa kasi wakihofia kukamuliwa kiuchumi, ingawa mara nyingine hofu yao hii huwa sio ya kweli. Inasemekana baadhi ya wanawake wa aina hii huwekeza zaidi kwenye kuonekana wazuri na walimbwende ili kuficha au kufunika baadhi ya mapungufu yao.

Wanaume wengi walioulizwa sababu za kuwatumia na kuwatelekeza wanawake wa jinsi hii walisema kuwa, kwa kutembea, kuonekana nao au kufanya nao mapenzi, wanaume hawa hujihisi sifa sana, hususani wanapoonekana na wanaume wenzao, yani ni kama vile timu ndogo iliyopata nafasi kucheza katika kombe la dunia. Unajua tena wanaume wanavyopenda kujionyesha wanapokuwa na wanawake wazuri mbele ya macho ya wanaume wenzao.

Wamesema kwamba wanapowaza kuishi na wanawake hawa kama mume na mke, huwa wanazidiwa na hofu ya kuelemewa au kujihisi kutokuwa salama “sense of insecurity”. Mioyoni mwao wanahisi kwamba kama wanaume wenye hela wamekuwa wanamfuatilia kwa kasi kubwa hivi mwanamke huyu, vipi nikishaoana naye?? Si ndiyo kila siku kusuguana na kukorofishana vishawishi vinapozidi? Je nitaweza kustahimili?

Wanaume wengine walioulizwa walijibu kwamba, wanawake wa jinsi hii ni wa gharama sana, sio rahisi kuwaweka mjini na kuhakikisha wanaishi maisha yao ya kawaida kama hauna fedha ya kutosha. Hata wale wanaume wachache waliokuwa na hao wanawake kwa muda wa maswali haya wameeleza jinsi wanavyohisi wanatumia fedha nyingi na yamkini zaidi ya wanavyojiweza.

Wanawake wa aina hii watahitaji mitoko ya nje ya mji, sehemu zilizojitenga, sehemu za faragha ambazo ni za bei ghali, wanataka zawadi za gharama, ukitaka kuwapa zawadi za kushtukiza “surprise” basi ujipange, sio vitu vya kitoto vitakavyomsisimua aweze kukwambia “waoooooow…this is wonderful” hapo lazima ujipinde mfukoni haswa.

Ukitaka kuwatoa nje kwa ajili ya chakula cha jioni basi lazima kwenda maeneo wanayoenda watu maarufu, mkitaka kwenda kupumzika kidogo nje ya nyumbani basi uwaambie wachague wao wapi pa kwenda, na hapo utakapotajiwa ni pa gharama kubwa sana, na imeelezwa kwamba pamoja na mambo yote haya ya gharama kubwa bado huko wapenzi hawa wanapoenda msichana huyu anaishia kuonekana ni mwanafunzi asiyejua tendo la ndoa kabisa tofauti na hali aliyoionyesha “poor perfomer”, wanaume wengine wanasema inaonekana kama kupoteza tu pesa, unaishia kutokufurahia penzi lenyewe.

Na wengine wameenda mbali zaidi kueleza kwamba hata unapotaka kuzaa na mwanamke wa jinsi hii basi yeye anataka mtoto mmoja au wawili tu akiogopa asije kuliharibu umbo lake, tofauti na kiu ya mwanaume ya kupata watoto zaidi ya wawili. Imeelezwa kuwa hata ujuzi wa kupika kwao ni shida maana kutwa kucha wako “bize” na sura zao, na hata ukikaa nao sio watu wakufurahisha zaidi ya kutumia tu hela zako “they are boring”.

Pamoja na uchunguzi huu na ukiangalia hali halisi ya maisha yetu ya kila siku tena katika jamii tofauti utagundua kwamba wanaume kiu yao sio kuoa wanawake wenye umaarufu, au wenye kujulikana sana, au walio warembo kupindukia, bali wanaume wanapotaka kutafuta mke wa kuoa wanaangalia tabia na haiba zilizojificha, wanauliza tabia ya huyo msichana, wanataka kujua anavyohusiana na watu, wataangalia nyendo zake kuanzia wakati anasoma.

Ni ngumu kuwakuta wamenaswa na aina ya wanawake ambao wanataka kuonekana wakati wote, wanataka wajulikane kuwa wao nao wapo kwenye makundi ya watu, la hasha. Kiu zao ni kuwa na mwanamke ambaye atakuwa mke anaye leta furaha nyumbani, anaye sikiliza, anaye weza kushauri na kushaurika, aliyeko tayari kufundishika sio kuwa mwalimu kwenye kila kitu, anayeweza kuandaa mapishi mazuri yatakayo wafurahisha watoto na mume wake, sio kila siku kuelekeza kipikwe nini wakati yeye analinda kucha zake zisiharibike.

Hivi umewahi kujiuliza kwanini watu wengi waliooa wakiwa na michepuko, hiyo michepuko ni mabinti warembo na walimbwende ila hawajaolewa, hivi hujajiuliza kwanini hawajaolewa? Na hata wengine wakiolewa hizo ndoa kila siku tia maji tia maji, wataachika leo na kuolewa kesho na kuachika kesho kutwa nakuolewa tena mtondogoo.

Unadhani hawa wanaume wanaoenda kwa hao wanawake ni kwamba hawajui wanachokitaka? utashangaa hata umpe mapenzi gani bado hawezi kukwambia atakuoa, ingawa yuko tayari akupangishie nyumba au hata akujengee lakini ulale huko mwenyewe, yeye anaenda kulala na mke wake. Ushauri wangu wa bure kwa wanawake wa jinsi hii; badilikeni tabia zenu, jitihada mnazotumia kwenye kucha na sura zenu ziwekeni kwenye kushuhulikia tabia na haiba zenu, la sivyo mtasubiri sana tu.

Dr. Chris Mauki
UDSM & University of Pretoria. SA
chrismauki57@gmail.com


==>Kandili244

BAADA YA MIAKA SITA LADY JD AMTEMBELEA RAY C...SOMA KILICHOENDELEA...

 
Mwanamuziki Mkongwe Lady Jay Dee Amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuonana na Mwanamuziki Ray C ambae yuko katika harakati za kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya........

From @jidejaydee - 
Thank you for visiting me doll( Ray C)
A message of Hope:
Kila Mtu Anapitia Magumu Katika Maisha
Kwa Njia Tofauti
Hakuna Jaribu Lisilo na Mlango wa Kutokea, Amini na Amua
Nakupa Moyo na Mungu Akusaidie
Kwa Yote Unayopitia
Akuondolee Akuepushie
Na Akupe Kufahamu na Kukiri Mabaya 🏼🏼🏼🏼🏼🏼
Watu Wanakupenda
Nakumbuka Tulivyo Anza
Kimtindo nai miss Competition
Pls Come Back
Naamini Bado Unayo Nafasi
Binti Amka Jikaze Anza Mwendo
Umrembo na Bado Wang'ara 🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻
Ni baada ya miaka 6
Tangu kuonana mara ya Mwisho
Story nazo ni ndefu na nyingi

Ombi:
Tuheshimu na kuhurumia matatizo ya wengine, tafadhali msi comment vibaya wala kwa kejeli.
Lolote linaweza kumfika yoyote
SAA yoyote
Tuonyeshe Mapenzi

KILICHOIPONZA SIMBA FA CUP HIKI HAPA,SOMA ZAIDI,VIONGOZI WANENA MAZITO....

Baada ya michezo mitatu ya Kombe la FA kuchezwa na kushuhudia timu za Dar es Salaam Young AfricansMwadui FC na Azam FC kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, April 11 2016 ilikuwa zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga.
Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Coastal Union kutokana na timu hiyo kuaminika kuwa chini ya kiwango naSimba kuutawala mchezo, wamekubali kipigo cha goli 2-1 wakiwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
DSC_0041
Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 20 naYoussouf Sabo aliyefunga kwa mpira wa faulo. Simba walifanya mabadiliko na kumuingiza Hamis Kiiza ambaye alifunga goli la kusawazisha dakika ya 50 na kuufanya mchezo kuwa sare hadi dakika ya 85 Youssouf Sabo akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyotokana na makosa na Novat Lufungo kumchezea faulo Shiboli.

ANTI EZEKIEL ATUMBULIWA JIPU,KAULI YA JPM YAMTUMBUA JIPU...SOMA KISA KAMILI...

aunty-ezekiel34 
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.
Dar es Salaam: Mnyoosho! Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.
Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.
aunt-audi
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Aunt kutaka kujua kisa kamili ambapo alipobanwa alikiri kukamatwa kwa gari lake hilo kwa makosa ya kukwepa kodi wakati linaingizwa Bongo hivyo kuwa mikononi mwa TRA.
“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.
aunt-audi1“Nilishtuka sana baada ya kukamatwa kwani nilihisi ndiyo mwisho wa kuwa na gari langu lakini sasa nimepata moyo baada ya kuambiwa hakuna kilichochakachuliwa.

“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’ huku akigoma kutaja bei yake.

==>KANDILIYETU244

JAMAN MAPENZ JAMANI,SOMA HII KALI,WANASEMA MWANZO,KATI HADI MWISHO NI...

Mpenzi msomaji wa XXLove, tunakutana Jumatatu nyingine kwa rehema za Mwenyezi Mungu. Wiki hii tutaangazia hisia za kimapenzi zinavyotakiwa kuoneshwa kwa wapenzi. Hisia hizo zinatakiwa ziwe mwanzo, kati na mwisho na si katikati tu wakati wa tendo husika kama wafanyavyo wengi. 
Mapenzi ni hisia. Hisia zilizojaa utamu ndani yake. Hisia zenye raha na mshawasha wa ajabu, ambao wahusika wanapaswa wawe nazo. Hisia hizi zinatakiwa zionekane kabla (mwanzo), wakati wa tendo lenyewe na hata baada ya tendo. Siyo kukurupuka kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya.

Kimsingi mwanamke anapaswa aoneshe hisia zake kwa mwenza wake kabla hata hawajaingia kwenye uwanja wa mechi. Kama mihemko na hisia zako ziko jichoni ndiyo ulirembue sasa hilo jicho, mtoto wa kike uoneshe utofauti wako na mwenza wako. Kama ni joto la mwili kuongezeka na uliache basi liongezeke. Kama ni pumzi nyingi kushuka, ziache zishuke. Kama ni kupumua kama umekoswakoswa na mkuki basi acha upumue.

Vivyo hivyo kwa mwanaume, mapenzi hayahitaji haraka wala papara. Utamu wa mapenzi ni maandalizi ya mwili, akili na mazingira.
Kama mtaruhusu miili yenu kuonesha hisia za mapenzi mlizonazo, hata kwa kumwangalia tu mwenza wako, unajikuta ukipata hisia kali sana ambazo zinakufanya usikie utamu wa kile kinachoenda kutokea.
Hisia ninazozungumza hapa ni zile zinazomtofautisha mwanamke na mwanaume. Hisia ambazo huonekana au hutokea wakati wapenzi wanapokuwa faragha.

Wanaume wengi wanaonekana kuwa na haraka sana wanapokuwa katika uwanja wa mahaba na wanashindwa kuwaandaa wenza wao na kutaka kufakamia tu tunda bila hata kuliosha au kulimenya kwanza pasipo kufahamu kuwa maandalizi ya awali ndiyo yatakayokusaidia mwanaume na mwanamke kuweza kufikishana kwenye kilele cha mafanikio.

Cha kufahamu msomaji ni kwamba hisia za baadhi ya wanawake ziko mbali sana tofauti na mwanaume hivyo ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha anazifukunyua zilipo. Naye mwanamke ni wajibu wake kuhakikisha anajirembua kadiri awezavyo ili kumruhusu mfukunjuaji aweze kuzifukunyua hisia hizo.

Hisia za kati ni zile zinazotokea au kuonekana wakati wa tendo husika. Mwanamke anapaswa atimize anachopaswa kukifanya na hata mwanaume naye anapaswa afanye yale apasayo kufanya kwa mwenza wake.

Hisia za mwisho ni mara baada ya tendo lenyewe. Mwanamke au mwanaume anapaswa kuendelea kuonesha hisia kwa mwenza wake kuwa bado anampenda, anamthamini na bado anatamani muda ungekuwepo waendelee na ‘kindumbwendumbwe’ chao.
Mpenzi msomaji usikose sehemu ya pili ya makala haya wiki ijayo.
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top