Social Icons

Loading...

Lowassa asema ushindi wake ni mkubwa...Asema hajabahatisha kuomba nafasi ya Urais...

Lowassa akihutubia

MGOMBEA urais wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowasa, amesema nafasi yake ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25, mwaka huu ni kubwa kutokana na Watanzania kukichoka chama tawala CCM.

Alisema dhamira yake ya kuomba nafasi ya urais si ya kubahatisha bali kazi hiyo anaijua na kuiweza; hivyo akiingia madarakani, ataboresha maisha ya Watanzania, kukuza uchumi na kuharakisha maendeleo.

Lowassa aliyasema hayo Mjini Bunda, mkoani Mara jana na kuwaahidimabadiliko makubwa ya kilimo cha kisasa wakazi wa mji huo kama wakimpakura za kutosha ambazo zitamwezesha kuingia madarakani.

"Nitakuza uchumi wa mkoa huu kwa kilimo cha umwagiliaji, mtatumiamaji ya Ziwa Victoria kujinufaisha...kipaumbele changu cha kwanza ni elimu kikifuatiwa na kilimo, nitaweka mkakati wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya maji katika Mto Nile.

"Lengo langu ni kuhakikisha Watanzania hasa wanaoishi karibu na Ziwa Victoria, wanafaidika na kilimo cha umwagiliaji...naomba mnipigie kura Oktoba 25, mwaka huu niwe rais wenu mpate mabadiliko, nataka tuondokane na umaskini uliokithiri," alisema.

Alisema Serikali yake itatumia fedha zitokanazo na madini, gesi namaliasili za Taifa letu ambazo hazijamnufaisha Mtanzania.

Mzee Hamisi Mgeja
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, mkoani Shinyanga aliyehamiaCHADEMA, Mzee Hamis Mgeja, alisema Lowassa ana dhamiraya kuleta mabadiliko ya kweli kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Alisema wote waliokimbia CCM ni wasafi na wachafu ndio waliobakina kuongeza kuwa, Serikali ya CCM ndiyo iliyoua Mashirika ya Ummapamoja na viwanda ambavyo awali vilikuwa vikizalisha kwa faida.

Akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMA, Jimbo la Bunda Mjini,Esta Bulaya, Mzee Mngeja alisema mgombea huyo ni chaguo la wanabunda kwa ajili ya mabadiliko.


author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top