November 11 millardayo.com ilifanya exclusive interview na kiungo wa kimataifa waTanzania anayecheza soka la kulipwa Malaysia katika klabu ya UiTM Abdi Kassim Sadallah ambaye amewahi kutamba katika vilabu kadhaa vya Ligi Kuu soka Tanzania bara ikiwemo Yanga, Azam FC pamoja na Mtibwa Sugar.
Abdi Kassim ambaye pia anafahamika kama Babi au Ballack wa Unguja anacheza katika klabu ya UiTM inayomilikiwa na University of Technology MARA cha Malaysiaamemaliza mkataba na klabu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2014 hivyo amegoma kuongeza mkataba mpya kwanza akitafakari ofa aliyopewa.
Kiungo huyo ambaye bado yuko Malaysia licha ya kuwa Ligi Kuu imemalizika huku yeye akiwa kacheza mechi zote 22, kufunga magoli 7 na kuisaidia klabu yake UiTM kumaliza nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi Kuu Malaysia, bado hajakubali kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo kutokana na timu hiyo kutofikia dau analolitaka hivyo bado anatafakari ofa hiyo hadi mwezi January au February 2016 au anaweza kutimkia Indonesia.
“Kiufupi Ligi imemalizika na mimi mkataba umemalizika kwa hiyo sasa hivi ninachoangalia connection tofauti tofauti hapa Malaysia na Indonesia kwa hiyo sasa hivi nipo likizo nategemea kuja Tanzania kuona familia lakini nina mipango ya kurudi Malaysia January au February nitarudi tena kuendelea na soka au naweza kwenda Indonesia” >>> Abdi Kassim
Post a Comment