Social Icons

Loading...

CHEKI RAMANI YA LUTENI KALAMA SOUTH AFRIKA...JE STEVEN NYERERE NA JB WAMEPEWA SUMU??SOMA MAJIBU YA DAKTARI HAPA...

Gangwe Mob ni kundi ambalo kama ukiitaja safari ya Bongo Fleva Tanzania, huwezi kuacha kulitaja kundi hilo lililoundwa na Luteni Kalama pamoja na Inspector Haroun.
Luteni Klaama
Luteni Kalama na Inspector Haroun
Luteni Kalama amesimulia kwamba kuna time alikuwa na mipango ya kuzamia South Africa, rafiki yake mmoja alimchorea ramani ya safari nzima mpaka atakapofika.
Baada ya kukutana na Inspector Haroun alimshirikisha kuhusu mipango yake hiyo huku wakiendelea kufanya shughuli za muziki… Kalama anasema baadae ramani yake ilipotea kwa hiyo hata mpango wa safari haukuwepo, lakini baada ya muda alikuja kujua kwamba kumbe ramani yake haikupotea ila Inspector Haroun aliificha !! Mipango ya safari ikaishia hapo wakaendelea na muziki.
JB
Mwigizaji JB
Kuna stori kuhusu Steve Nyerere na JB kulishwa sumu, na ishu inahusishwa na Uchaguzi, kuna ukweli ??
JB amesimulia ilivyokuwa kwamba walikuwa pamoja wakala chakula kwenye sehemu tofauti… baadae JB amesema aliumwa sana tumbo akaamua kwenda Hospitali, baada ya kufanyiwa vipimo alipatiwa matibabu.
Mwigizaji Steve Nyerere
Mwigizaji Steve Nyerere
Kuhusu ishu ya sumu, JB amesema haamini kama chakula hicho kilikuwa na sumu ila alichoambiwa Hospitali  ni kwamba chakula kilikuwa kibovu na tayari amepatiwa matibabu japo maumivu ya tumbo aliyoyapata yalikuwa makali sana.
Chillah Bpoy
Q Chief
Q Chief na Harmonize ndani ya studio, walishirikiana kufanikisha mdundo wa Q Chief?Harmonize alisimulia kwamba alishiriki kuandika verse moja ya wimbo wa ‘Mdogo Mdogo‘ wa Q Chief, leo 255 iko na Chillah mwenyewe ambaye amesema ni kweli kuna mawazo ya Harmonize yalioyosaidia kukamilisha verse ya pili kwa sababu wakati ngoma hiyo inafanywa walikuwa pamoja studio.
Harmonize
Harmonize
==>>Millardayo.com

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top