Ni saa chache tu zimepita toka Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli aapishwe na kuanza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan… mpya nyingine ni juu ya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu anayeanza majukumu yake mapya kwenye Serikali ya tano inayoongozwa na ‘Tingatinga Magufuli‘
Kazi imeanza, Rais Magufuli amemteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kesho November 06 2015 ataapishwa Ikulu Dar es Salaam.
Mwanasheria huyo sio mgeni kwenye nafasi hiyo, George Masaju alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyomaliza muda wake iliyoongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambapo aliishika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anaongoza wakati huo, Jaji Frederick Werema kujiuzulu December 2014 wakati wa sakata la ESCROW
Post a Comment