Kwenye list ya Wabunge wa upinzani ambao waliwahi kugusa vichwa vya habari na kutikisa Vikao vya Bunge lililopita Tanzania, David Kafulila wa Chama cha NCCR- Mageuzi yumo !! YES.. Na kilicholiongezea uzito jina lake ilikuwa ishu ya ESCROW, ambayo ilipelekea baadhi ya Mawaziri kuachia nafasi zao pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Lakini jina lake pia halipo kwenye list ya Wabunge ambao tunatarajia kuwashuhudia kwenye Bunge jipya litakaloanza baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika, sababu inayopelekea hilo ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha hakupata Kura za kutosha ili awakilishe watu wake wa Kigoma Kusini Bungeni.
Kinachoendelea kwa sasa ni hiki kuhusu Ubunge wake >>>”Mpaka sasahivi ni suala ambalo linafanyiwa kazi na Mwanasheria anayeitwa Mpare Mpoki… Jumatatu ya wiki ijayo Kesi tutaiingiza Mahakama Kuu Tabora.”- David Kafulila.
“Ni kesi ambayo inatakiwa kuandaliwa kwa weredi mkubwa kuepusha mapungufu, lakini ni kesi fupi kwa sababu tunachokitaka ni ifahamike kwamba aliyetangazwa siye aliyeshinda.” >>> David Kafulila.
Kuna ushahidi unatakiwa? >>> “Hatuhitaji mlolongo wa mashahidi isipokuwa fomu za Matokeo… Nilishinda mimi kwa kura 34,000… nawahakikishia Wananchi wa Kigoma Kusini kwamba Kura zao haziwezi kupotea, Wataongozwa na Mbunge ambaye walimchagua.” >>> David Kafulila.
“Tume tuliyonayo ya Uchaguzi haijawa huru na ndio inapelekea mapungufu kujitokeza… Kuna kasoro nyingi za Uchaguzi, ni matokeo ya mfumo… Kuna taarifa kwamba kulikuwa na maelekezo toka Ikulu kwamba mpinzani wangu atangazwe mshindi kwa sababu niliambiwa niachane na ESCROW lakini sikukubali” >>> David Kafulila
Post a Comment