Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kwenda Ikulu iliyokuwa inamkabili mbunge mteule wa Jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee (35) na wenzake wanane, kwa kuwaachia huru kisha polisi kuwatia mbaroni tena. Kesi hiyo ilifutwa jana na Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda akisema mahakama hiyo haioni haja ya kuendelea nayo kwa sababu hakuna mashahidi wa kuithibitishia kama walitenda kosa hilo. Hakimu Kaluyenda alitoa uamuzi huo baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kudai kuwa kesi hiyo ilifikishwa jana kwa ajili ya kusikilizwa, lakini shahidi ambaye ni Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro hakufika mahakamani hapo kwa kuwa alikuwa amefiwa. Hakimu alisema kutokana na mashahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuhudhuria mahakamani, anafuta kesi hiyo na
kuwaachia huru washtakiwa hao. Alifafanua kuwa washtakiwa hao wameachiwa huru chini ya Kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Hata hivyo, alisema kifungu
hicho kinaruhusu upande wa mashtaka kuwakamata washtakiwa hao pale watakapoona inafaa na hata
kuwashtaki. Naye mdhamini wa Halima Mdee alidai kuwa mshtakiwa huyo, ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa. Alipotakiwa kuthibitisha
madai hayo kwa kutoa cheti cha daktari, alidai hakukabidhiwa.
Post a Comment