Ikiwa jiji la Dar Es Salaam kwa upande wa wapenda soka wote wanautazama au kuusubiri mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018 Urusi, mchezo ambao utahusisha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya AlgeriaNovember 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, majirani zao Uganda walisafiri hadi Togokucheza mechi yao dhidi ya timu ya taifa ya Togo mechi ambayo imechezwa November 12.
Kwa upande wa Togo ambayo nembo yake kubwa ni Emanuel Adebayor ambaye hakuwepo kikosini walikubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Uganda The Cranes, Togoilikuwa na nyota wake kadhaa pamoja na beki wa kati wa Yanga Vincent Bossouambaye hakucheza mchezo huo wakati Uganda wakiwa na nyota wao mahiri kamaHamisi Kiiza na Juuko Murshid wanaoichezea Simba walifanikiwa kuwafunga Togo.
Goli pekee la Uganda The Cranes lilifungwa na Farouk Miya dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90 za mchezo na kuwafanya waganda hao watoke nje ya uwanja huku wakitabasam.
Haya ni matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 zilizochezwa November 12
Post a Comment