Naamini kuna watu wangu ambao wanatamani wapate walau dakika tano kuchill na mastaa kadhaa wanaowakubali, kuwauliza maswali tofauti kuanzia maisha, biashara, muziki ama sanaa yoyote ile wanayoifanya… lakini umeshawahi kukaa na kujiuliza wasanii au mastaa wanakaa na kutamani vitu gani?
Nimetembelea mtandao wa Twitter na huko nimekutana na #hashtag inayoweka headlines kwenye matumizi yake kwa siku kadhaa sasa, yenyewe inaitwa#ThingsILongThroatFor ambayo mastaa wengi wakubwa wa Africa wamekuwa wakiitumia kuvitaja vitu ambavyo wangetamani kuwa navyo!
Kwenye mchezo huu wapo wengi walioshiriki, baadhi yao wakiwa Wizkid, Tiwa Savage, Seyi Shay na wengine… Je, unajua Wizkid anatamani kuwa na nini ama kuwa nani siku moja? Tiwa Savage je? Zote zimejibiwa kwenye hizi tweets chache nilizofanikiwa kuzinasa kupitia account zao za Twitter.
karibu uzipitie moja baada ya nyingine kisha uniambie hapa chini kwenye comment, ni vitu gani unatamani uje kuwa navyo ama ni mtu gani ambaye ungependa kuspend nae time hata kama ni kwa siku moja.
Post a Comment