Brazil ni nchi ambayo kila mpenda soka anaifahamu kwa kutoa vipaji vingi katika soka, katika mfumo wa uzalishaji wachezaji Brazil ni tofauti kidogo na nchi za Ulaya, asilimia kubwa ya wachezaji wazuri kutokea Brazil ni watu ambao wamejifunzia soka mtaani.Brazil ni nchi yenye idadi ya watu milioni 200 lakini asilimia kubwa ya vijana hupenda kujihusisha na mchezo wa soka. November 9 naomba nikusogezee tabia 5 za wachezaji wengi wa kibrazil ambazo wanatajwa kuwa nazo.
1- Ni aina ya wachezaji ambao hupenda kucheza soka nchini kwao, wachambuzi wengi wa masuala ya soka hupenda kusema kuwa wachezaji wa kibrazil huwa wanaumwa homa ya kupenda nyumbani, kama utakuwa unakumbuka vizuri kabla ya Neymarkujiunga na FC Barcelona kulikuwa na mjadala mrefu sana katika baadhi ya vyombo vya habari ambavyo wanaamini Neymar anapaswa kwenda Ulaya na wengine kusema hataBrazil anaweza kuwa mchezaji bora.
2- Wengi wao hutokea maisha ya mtaani na asilimia kubwa mara wapatapo pesa hupenda kufanya starehe kitu kinachotajwa kuwa ni tabia ya kujisahaulisha matatizo. Baadhi ya mastaa wa Brazil wanaotajwa kupenda starehe ni Ronaldinho Gaucho.
3- Ni watu ambao hupenda kujivunia utamaduni wao na kudumisha aina ya muziki wao wa asili Samba hata tumewahi kuona mara kadhaa wakifunga magoli hupenda kushangilia kwa kucheza staili hiyo ya muziki.
Post a Comment