Ni siku chache tu zimepita tangu mnyange aliyevaa taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, amwage mambo hadharani kuwa alijinunulia gari jipya kabisa la bei mbaya. Wema alisema katika sherehe yeke ya siku ya kuzaliwa kuwa alitumia pesa zake mwenyewe kununua ndinga hilo aina ya Range Rover Evogue 504 lenye thamani ya dola za Marekani zaidi ya 90,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 190 za Tanzania.
Gari aina ya Range rover Evogue 504 la Wema Sepetu
|
Akinukuliwa na kampuni ya habari ya Global Publishers, mtu huyo ambaye hakupenda jina lake liwekwe hadharani alisema kuwa Wema alipewa gari hilo na mwanaume mmoja raia wa Kongo ambaye awali alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mnyange mwingine anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini Tanzania, Jackline Wolper.
Wema Sepetu katika 'Birthday party' yake |
"Nasikia lile gari, kwanza kweli ni jipya. Lakini liko kwa dalali sokoni. Sasa watu wanaojua habari za mjini wanasema kuwa, Mkongo aliongea na dalali, wakaelewana kwa kumpa pesa kidogo, zikatengenezwa dokyumenti ambazo zinamwonesha Wema kuwa ni mmiliki halali wa gari," kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa kwa njia ya simu ili kufafanua jambo hilo, Wema aliomba muda ili aweze kuuongea kwa nafasi. Hata hivyo mrembo huyo hakupokea tena simu na wakati mwingine hakupatikana hewani
==>www.bilawaa.com
Post a Comment