Social Icons

Loading...

ADELE AMTEMA BEYONCE KWENYE COLLABO...SABABU ZA KUTEMWA HIZI HAPA...NAE AFUNGUKA KUHUSU HATUA HIYO...

Msanii yoyote akifatwa sasa hivi na kuambiwa Beyonce anataka kufanya collabo na wewe..” kwa asilimia mia jibu litakuwa ndio tena kwa herufi kubwa NDIO!! Lakini hii sio ndoto kubwa kwa msanii wa muziki wa Pop kutoka UingerezaAdele.
Kwa mujibu wa baadhi ya mitandao ikiwemo mtandao wa Yahoo Celebrity News, umeripoti kuwa Beyonce amekuwa akiomba kufanya kazi na staa huyo wa Uingerezakwa takribani mwaka mzima lakini juhudi zake hazijawahi kuzaa matunda, inaripotiwa pia kuwa, Beyonce alishaingia studio na Adele na kujaribu kumshawishi staa huyo kurekodi nae wimbo mwaka jana lakini bado Adele akamtolea nje.
BEYADELE2
Adele & Beyonce Knowles.
Licha ya hayo, tunaambiwa toka kipindi hicho Beyonce amekuwa akijaribu mara kwa mara kubadilisha mawazo ya Adele ili kuingia naye studio, lakini kila mara anapojaribuAdele anakataa, kitendo kilichompelekea Beyonce na yeye kufanya maamuzi ya kuirekodi single hiyo mwenyewe na kuiweka kwenye Album yake mpya inayotegemea kuwa mtaani mwshoni wa mwaka 2015.
>>> “ Bey amekuwa akimuomba Adele kwa kipindi kirefu kuingia naye studio na pamoja kuweka historia nyingine kwenye muziki, akafanikiwa kumleta studio lakini alipojaribu kumshawishi kuhusu kurekodi naye wimbo Adele alikataa kabisa, kwahiyo Beyonce naye ameamua kuuweka wimbo huo kwenye Album yake mpya, na inawezekana Album hiyo ikatoka mwisho wa mwaka huu” <<< source karibu na Beyonce aliuambia mtandao wa Heat Magazine.
BEYADELE3
Adele.
Na kwa mujibu wa mtandao wa International Business TimesAdele ametoa sababu za yeye kukataa kufanya kazi na Beyonce Knowles
>>> “ Nadhani kazi zake na historia yake kama msanii na muimbaji inaogopesha na kutoa changamoto kubwa… lakini watu wengi wanaonivutia mimi na ambao ningependa kufanya nao kazi ni watu wa old school music na kwa bahati mbaya wote wametangulia mbele za haki, isitoshe zivutiwi na umaarufu kwasbabu naogopa umaarufu unaweza kunipoteza kimuziki na vilevile kuwaumiza familia pamoja na watu wangu wa wakaribu, mpaka hapa nilipofika bado napata shida kuzoea” <<< Adele.
BEYADELE4
Adele na Beyonce ni wasanii wawili ambao ushawishi wao duniani ni mkubwa sana na licha ya wao kufanya aina mbili tofauti za muziki, mastaa hawa wameweza kupata umaarufu mkubwa kwa kusimama peke yao kimuziki na licha ya mashabiki wao kuonekana kuvutiwa na wazo la wawili hao kufanya collabo, tunaambiwa Beyonce hana kinyongo na msanii huyo.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top