Social Icons

Loading...

LISU KUMRUDISHIA KAFULILA UBUNGE WAKE MAHAKAMANI...JE ATAFANYAJE SOMA MBINU ZOTE HAPA...

 Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR -Mageuzi, David Kafulila, amewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasna Mwilima.
 
Akizungumza na Nipashe jana baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema amefungua kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 ya uchaguzi, akiwalalamikia Mwilima, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa serikali.
 
Alisema kesi hiyo itasimamiwa na mawakili wawili, Tundu Lissu na Daniel Lumengela, huku hoja ya msingi katika shauri ikiwa ni kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo anadai si halali kwani kutokana na fomu 382 za vituoni na kusainiwa na wasimamizi na mawakala, alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake (Mwilima)

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top