Tayari tuna stori kuhusu Mchekeshaji Masanja kushindwa kwenye Ubunge Jimbo la Ludewa ambapo matokeo ya kura za maoni yameonesha jamaa anashika nafasi ya tatu… Masanja amesema kashindwa lakini anajipanga kwa mara nyingine kwa ajili ya kusimama kwenye Ubunge mwaka 2020.
Masanja amesema kitu kingine ambacho alikutana nacho na hakutegemea ilikuwa mfumo wa Kura za maoni, alidhani wanaCCM wote Ludewa watapiga Kura lakini utaratibu ukawa tofauti, viongozi pekee ndio waliopiga Kura kupitisha jina la mgombea Ubunge wa CCM ambapo Masanja hakufanikiwa kupita
Post a Comment