Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbroad Peter Slaa amezionesha stakabadhi za malipo ambayo Lowassa aliyafanya ili kujiunga na chama hicho, Dr. Slaa amesema kuwa amefikia hatua hiyo ili kuwaonesha Watanzania kile kilichomfanya yeye kuondoka CHADEMA. Ameendelea kusema kuwa pia amesukumwa kufanya hivyo ili kuwaonesha wana CHADEMA waliokuwa wanambeza na kusema kanunuliwa ili mara nyingine wasirudie kusema mambo wasiokuwa na uhakika nayo.
Akiongea mbele ya vyombo vitatu vya habari akiwa mjini Austin, TX nchini Marekani ambako anachukua kozi fupi ya Sheria ili kujikumbusha vitu vilivyobadilika kwenye fani hiyo ambayo anatarajia kuanza kuifanyia kazi kuanzia Januari mwakani.
Nyaraka hizo za siri za CHADEMA zimezua gumzo kubwa nchini humo na watu wengi waliopata kuziona wameibeza sana CHADEMA na kuifananisha na chama cha Kidalali, chama cha wapiga pesa alisema Injinia Musa Kipao mkazi wa Tabata jijini Dar.
==>>http://njoohuku.blogspot.com/
Post a Comment