Social Icons

Loading...

MSHINDI MTANZANIA WA SHINDANO LA TRACE MUSIC STARS AFRICA HATIMAYE SAFARI YAKE YA KUKUTANA NA AKON...SOMA ALICHOKISEMA...

Mshindi wa shindano la Trace Music Stars Africa, Mtanzania Nalimi Mayunga anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za Bongo Fleva. Baada ya kushinda shindano hilo kubwa la kusaka vipaji, Mayunga aliondoka na mkataba wa kurekodi naUniversal Studio wenye thamani ya dola 500,000 ambayo kwa pesa ya sasa inagonga mpaka Tzs bilion 1!
MAYUNGA2
Good news kwako mtu wangu, mtu wetu Mayunga anatarajiwa kuondoka Tz siku yaJumatatu tarehe 16 November 2015 kwenda Marekani kwa ajili ya mafunzo ya muziki pamoja na kurekodi single yake na Akon ambaye kwenye shindano la Trace Music Stars Africa alikuwa miongoni wa majaji.
MAYUNGA3
Akiongea na CloudsFM radio leo kupitia kipindi cha XXL, Mayunga aligusia pia kuhusu safari yake ya Marekani
>>> “Marekani naenda Jumatatu na ninachoenda kukifanya kule ni kile kinachoongelewa kwenye media, kuwa naenda kwa ajili ya mafunzo, kufanya wimbo, na vilevile kushoot video ya wimbo nitakaoenda kuurekodi… japo kusema kweli sijajua wimbo huo utakuaje kwa sababu mpaka sasa bado sijaupata na wala sijausikia. Dili ni kwamba Akon anakuandikia wimbo mwenyewe, sema sijaupata ili niweze kujipanga, so nahisi kama anataka kunipima aone uwezo wangu… <<< Mayunga

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top