Social Icons

Loading...

UKAWA WAANIKA WAZI STAHILI YA KUMPOKEA RAIS MAGUFULI BUNGENI SOMA HAPA UONE IYO STAHILI...

Image result for MBOWE+MBATIA+LISSU+MAALIM SEIF
Dalili ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia Bunge zimeanza kuonekana, baada ya Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kumwandikia Spika wa Bunge la 11 kutaka ufafanuzi wa masuala matatu, kabla ya Rais Dk. John Magufuli, kuhutubia na kulizindua Bunge, kesho.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema hawatakubali kuvikanyaga viapo vyao walivyovitoa kwa kutumia vitabu vitakatifu vya kuilinda na kuitetea Katiba, kwa kuruhusu Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kuingia bungeni.
 
Katika barua hiyo ambayo imesainiwa na wabunge 98 wa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF, imeleza mambo matatu ambayo wanahitaji Spika kuyatolea majibu kabla ya kufikia uamuzi wao.
 
Aliyataja mambo hayo kuwa ni haitakuwa sahihi kikanuni wala kikatiba, na haitakubalika na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kulihutubia Bunge na kulifungua rasmi bila uwapo ndani ya ukumbi wa Bunge, wa Rais aliyechaguliwa kihalali na wananchi wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, na makamu wake wawili wa rais.
 
Pia, haitakuwa sahihi kikanuni wala kikatiba, na haitakubalika na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Zanzibar, Dk. Shein, kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge kama Rais wa Zanzibar.
 
“Tunataka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na kuahirishwa hadi hapo rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar, yaani Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Saba wa Zanzibar,” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosomwa na Mbowe na kuongeza:
 
“Suala la kuheshimu matakwa ya Wazanzibari kwa kumtangaza Maalim Seif kuwa Rais wa Zanzibar linalihusu Bunge na linatuhusu sisi Wabunge wote. Hii ni kwa sababu, masuala ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar yamewekewa masharti katika sura ya nne ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano.” 
 
Alisema: “Sisi Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni hatuko tayari kunajisi kiapo cha utii kwa Katiba yetu ambacho tumekila muda mfupi uliopita kwa kuruhusu mtu au watu ambao hawajapata mamlaka halali ya kuendesha nchi ya Zanzibar kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kufungua rasmi Bunge hilo.”
 
Hata hivyo, alipoulizwa kama watatoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais Magufuli atakapokwenda kuhutubia na kuzindua Bunge, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, alisema kwa sasa wanasubiri barua yao ijibiwe na Spika ndipo wataamua la kufanya.
 
JAMES MBATIA
“Tusubiri ofisi ya Spika itujibu barua yetu, ni mapema sana kusema mpango wetu kwa siku hiyo, yote yatategemea barua itakavyojibiwa,” alisema James Mbatia, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
 
Mbatia alidai kuwa kwa sasa kuna mpango wa kudhuru, kuua na kujeruhi viongozi wa Upinzani na kwamba kwa sasa kuna mikakati inaandaliwa mjini Dodoma kudhuru baadhi ya wabunge kwa hofu kuwa watafanya fujo wakati wa Rais Magufuli kuhutubia na kuonya kwamba kwa kufanya hivyo, Serikali ya CCM itabeba lawama.
 
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, alisema wataendelea kudai Katiba mpya, baada ya awali kuchakachuliwa na kuwekewa mizengwe mingi.
 
“Tunachotafuta ni maridhiano, tumekuwa waungwana na kuonyesha uongozi ...hatukutana damu za Watanzania zimwagike, ndiyo maana tumewatuliza baada ya uchaguzi. Wana machungu mengi moyoni, tumeipenda zaidi Tanzanja na vyama vyetu tumeviweka kando,” alisema.
 
JUMA HAMAD OMARI
Mbunge wa Ole kwa tiketi ya CUF, Juma Hamad Omari, alisema kwa sasa Zanzibar imewekwa chini ya Jeshi, kwa kuwa muda wa kuongoza kikatiba wa Rais Shein ulikwisha Novemba 3, mwaka huu, na kinachotumika ni mabavu.
 
“Mizegwe ilianza kabla ya kupiga kura, watu 60,000 walioonekana ni wapinzani walinyimwa kuandikishwa, watu 100,000 walinyimwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali, wengine waliitwa marehemu na wengine wanaofahamika walishakufa siku nyingi majina yao yaliendelea kuwapo kwenye daftari,” alisema.
 
Alisema Dk. Shein alishindwa kwa kura 24,800 na kwamba majumuisho ya majimbo 54 yalionyesha uchaguzi ulikuwa huru na haki na waangalizi wa ndani na nje walithibitisha hilo.
 
Alisema  Oktoba 28, mwaka huu, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, alikuwa mafichoni na baadaye aliibuka na kufuta uchaguzi kwa matakwa yake na CCM.
 
“Hana nguvu kikatiba na kisheria kufuta uchaguzi, hii ni kunajisi Katiba, muda wa Baraza la Wawakilishi umeisha, hakuna serikali, tunachoona ni vifaru vya jeshi na wanajeshi mtaani,” alieleza.
 
TUNDU LISSU
Mnadhimu wa Bunge, Tundu Lissu, alisema kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano na ya Zanzibar, uchaguzi wa Zanzibar umetajwa kwenye Katiba na inashangaza uhalali wa Rais Magufuli wakati Zanzibar hakuna serikali.
 
“Bunge halijatimia, kuna Wabunge watano wa Baraza la Wawakilishi hawapo Bungeni, leo wabunge walioapa kuitete Katiba sasa wanakanyaga viapo vyao vya Biblia na Quran, na rais anaruhusiwa kuingia bungeni likiwa halijakamilika,” alisema.
 
Lissu alisema ili Bunge likamilike, ni lazima kuwe na wabunge wa majimbo, viti maalum, wabunge watano wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa kuteuliwa, na kwamba wote wapo akiwamo mmoja wa kuteuliwa, lakini wa kutoka Baraza la Wawakilishi wanakosekana.
 
Alisem uhalali wa Dk. Magufuli utategemea uhalali wa Maalim Seif na kwamba kama wanataka asihojiwe ni lazima Maalim Seif apewe haki yake ikiwamo kuapishwa.
==>IPPMEDIA

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top