Social Icons

Loading...

MAZUNGUMZO YA SHEIN NA MAALIM SEIF USIRI MKUBWA...SOMA HAPA KUPATA KINACHOENDELA...SEIF AFUNGUKA HAYA...


Mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yameendelea kutawaliwa na usiri mkubwa,  licha ya vikao vitatu kufanyika Ikulu, mjini Zanzibar chini ya Rais wa visiwa hivyo, Dk. Ali Mohamed Shein.

Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini hapa jana kuhusiana na mazungumzo hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hana taarifa yoyote kuhusu kilichozungumzwa na kuafikiwa.

Mazungumzo hayo yanashirikisha Dk. Shein ambaye alikuwa mmoja wa wagombea urais kupitia CCM, aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wastaafu wa kitaifa.

Vuai alisema chama chake hakifahamu chochote kilichozungumzwa katika vikao hivyo ambavyo vimekuwa vikiwashirikisha marais wastaafu akiwamo,  Ali Hassan Mwinyi, Aman Abeid Karume na Salmin Amour.

Alisema wakati mazungumzo hayo yakiendelea, chama chake kinaendelea kusubiri uchaguzi wa marudio kama ilivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kuwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu yamefutwa rasmi.

Alisema kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya CCM ni kuhamasisha wafuasi wake kushiriki kwa wingi katika uchaguzi utakapofanyika baada ya Zec kutangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi huo.

“Sisi tunachosubiri ni uchaguzi wa marejeo na tuna imani kuwa uchaguzi huo utafanyika kwani serikali haiwezi kupatikana bila ya kuwapo kwa uchaguzi,” alisema Vuai.

Kwa upande wa Cuf, nacho kimeeleza hakielewi chochote kinachoendelea kuhusiana na mazungumzo hayo ya kutafuta muafaka kumaliza mgogoro wa uchaguzi visiwani humo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Cuf, Ismail Jussa Ladhu, jana alisema usiri umetawala katika vikao hivyo kwani hata mgombea wao Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar hajawapa muhtasari wa mazungumzo hayo.

“Hadi sasa hakuna jipya usiri umetawala kwani hatufahamu chochote kilichozungumzwa katika vikao vilivyowakutanisha viongozi hao,” alisema Jussa.

Naye Katibu wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Issa Assakheri, alisema Maalim Seif anapohudhuria vikao hivyo huwa hatoi taarifa juu ya kilichozungumzwa katika meza ya pamoja.

 Msemaji Mku wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud, alisema serikali inasubiri tamko la Zec kuhusu tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio. Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejiandaa kwa gharama za uchaguzi huo ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya msingi kuchagua viongozi kwa njia hali za kidemokrasia.

Hali ya kisiasa Zanzibar imekuwa tete tangu Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, mwaka huu, kutokana na kutawaliwa na vitendo vya udanganyifu.

==>IPPMEDIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top