Tume ya Uchaguzi Tanzania NEC tayari imekamilisha kazi ya kuweka utaratibu mzima wa Uchaguzi mwingine wa Wabunge na Madiwani kwenye baadhi ya maeneo ambayo Uchaguzi haukufanyika.
Jimbo la Arusha Mjini nako Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo hilo haukufanyika baada ya Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mzee Estomih Jonas Mallah kufariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Ratiba ya Tume ya NEC imeonesha Uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Arusha Mjiniutafanyika December 13 2015… Kampeni zimeanza na hapa nina picha za Kampeni kwenye Jukwaa la Godbless Lema anayepeperusha bendera ya CHADEMA.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ nae ameunganisha nguvu kwenye Kampeni za Arusha kumsapoti Godbless Lema.
==>MILLARDAYO
Post a Comment