Baada ya klabu ya Azam FC inayoshindana kwa karibu na klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuwania nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi kutoa sare ya 1-1 dhidi ya African Sports January 16, katika mchezo uliochezwa Azam Complex Mbande Chamazi, January 17 ilikuwa zamu ya Yanga kuikabili Ndanda FC ya Mtwara uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Yanga ambao ndio wenyeji wa Ndanda FC katika dimba la Taifa, walikutana na wakati mgumu kidogo, kwani ngome ya ulinzi ya Ndanda FC haikuwa nyepesi kupenya washambuliaji wa Yanga, hadi dakika ya 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika matokeo yalikuwa 0-0.
Kipindi cha pili licha ya kutopata nafasi sana, Yanga walibadilika zaidi na kuhakikisha wanacheza katika eneo la Ndanda FC, mbinu ambazo ziliwapeleke Yanga kupata penati mbili, penati ya kwanza Yanga walipata, baada ya Simon Msuva kufanyiwa faulo katika eneo la hatari, laki Amissi Tambwe alikosa.
Hali bado iliendelea kuwa mbaya kwa Ndanda FC, kwani Yanga walikuwa tayari wana urafiki na eneo la 18 la Ndanda FC, kwani walifanikiwa kupata penati ya pili dakika ya 60 iliyopigwa na Kelvin Yondani na kutumbukia nyavuni, hadi dakika 90 zinamalizika Yanga1-0 Ndanda FC. Kwa matokeo hayo Yanga wanakaa kileleni mwa Ligi Kuu, kwakuwa na point 36 sawa na Azam FC lakini Yanga wamewazidi magoli Azam FC.
Post a Comment