Klabu ya TP Mazembe kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika sio furaha kwa wakongo wenyewe hata watanzania wamefurahishwa kuona TP Mazembe wakitwaa taji hilo huku kukiwemo na mchango wa wachezaji wawili wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Tanzania imezungumza sana na kufurahishwa na TP Mazembe kutwaa taji hilo huku mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu hiyo Mbwana Samattakuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga jumla ya goli nane na kumpiku mshambuliaji wa klabu ya Al Merreikh Bakri Abdel Kader Babeker.
Ushindi wa Mbwana Samatta haukuishia kwa watanzania wa kawaida na wapenda soka pekee hata Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete amezungumza kwa hisia kwa juhudi alizofanya Samatta na kutwaa kiatu cha dhahabu.
“Yaani amefanya vizuri sana hata mimi mwenyewe nasisimka angekuwa karibu ningempa mkono na kumwambia well done!! well done!! yule kijana ametupa sifa kubwa sana akijiunga na timu ya taifa itakuwa vizuri sana, kuhusu mechi na Algeria kinachotakiwa ni kushirikiana mwalimu amechagua wachezaji wazuri” >>> Jakaya Kikwete
Hata hivyo Rais mstaafu Dk Jakaya Kikwete aliwahi kuwatembelea Mbwana Samatta naThomas Ulimwengu wakati wakiwa Kinshasa katika kambi ya timu yao ya TP Mazembe. Pamoja na hayo Mbwana Samatta ambaye atajiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria utakaochezwa Jumamosi ya November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam amechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika itakayotolewa January 7 2016 Abuja Nigeria.
Post a Comment