Social Icons

Loading...

UZOEFU KATIKA SIASA:KUTANA NA MBUNGE MTEULE MWENYE ELIMU YA DARASA LA SABA AKIJIVUNIA MAMBO MATATU??JE MAMBO HAYO NI YAP?? SOMA HAPA?NI MBUNGE WA JIMBO GANI?NAWAAMBIA NINI WAPIGA KURA WAKE?TWENDE PAMOJA...

Kama hujawahi kukutana na kichwa cha habari kinamchomtaja Jumanne Kishimba, basi taarifa ikufikie kwamba kwenye list ya Wabunge wataowakilisha Dodoma kwenye Bunge la 11 na yeye yumo.
Jumanne Kishimba ni Mbunge mteule wa Jimbo la Kahama, lakini aliwahi kuandikwa pia kutokana na elimu yake ya darasa la saba !!
Kishimba
Jumanne Kishimba
Amepatikana kwenye exclusive interview na reporter wa millardayo.com, akaanza na stori kuhusu safari yake Kisiasa ilikoanzia >>> Nawashukuru sana wapiga Kura wa Kahama kwa kunichagua, nilijaribu mwaka 2000 wakati Jimbo la Msalala halijagawanywa lakini tulifutwa Wagombea wote wa CCM kulikuwa na rafu kidogo tulicheza. Toka mwaka 2000 sikuwahi kugombea mpaka mwaka huu 2015‘ >>> Jumanne Kishimba, Mbunge mteule Jimbo la Kahama.
Jumanne Kishimba (wa kwanza kulia) akisaini daftari la wageni.
Jumanne Kishimba (wa kwanza kulia) akisaini daftari la wageni.
Jumanne Kishimba aliwahi kuendelea kuiwaza Siasa baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza? >>> ‘Imekuwa kwenye ndoto zangu kwa kuwa biashara na siasa ni kama mtu na ndugu yake, kulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa elimu yangu ni darasa la saba lakini nina uzoefu wa kutembea sehemu nyingi na nimefanya kazi nyingi, ni vizuri kukawa na mchanganyiko wa wenzetu wenye elimu na sisi wenye uzoefu tukatatua changamoto pamoja Bungeni‘. >>>
Anazijua changamoto za wananchi wake? >>> ‘Wananchi wangu wanahitaji dawa, dispensary, maji, umeme.. ni vitu ambavyo elimu ya darasa la saba kwa Mbunge sio tatizo, Bungeni huendi kufanya operation kwamba unaweza kuua watu. Bungeni ninapeleka mawazo ya walionituma na kuongeza ya kwangu kwa kuwa una uzoefu‘. >>>Jumanne Kishimba.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top