Hali hiyo ilitokea jana wakati wa mkutano wa Chama cha Ushirika cha Siha Kiyeyo, kilichoko Sanya Juu, wilayani Hai, baada ya kuibuka kwa malumbano kati ya wanachama wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Alfred Morobo na Katibu wake Godfrey Masoki ambao wanatuhumiwa na baadhi ya wanachama kutosoma mapato na matumizi sambamba na kuwafukuza wanachama wanapohoji mali za ushirika.
Wakizungumza juzi katika kikao mara baada ya Nasha kuwa mwenyekiti wa muda, baadhi ya wanachama, Jackson Mwanri, Joackim Urio na Gadiel Munuo walisema wanashangazwa na kitendo cha Morobo kujimilikisha mashamba ekar tatu na Katibu wa Chama ekari mbili.
Mbali na tuhuma hizo, wanachama hao walidai kuwa Ofisa Ushirika Wilaya ya Siha, Fanuel Uroki na watumishi wenzake wawili, ambao hawakutajwa majina, wamepewa mashamba ya kulima huku wanachama wengine wakinyimwa.
Mwanri alisema kitendo cha Morobo kuwasimamisha uanachama baadhi ya wanachama, ni cha uongozi wa kimabavu na anaalikwa kwenye mkutano na kutia saini posho kisha kwenda hadi Morogoro lakini akifika tu anarudi. Alisema wanachama wakihoji arudishe fedha, anawafukuza au kuwasimamisha kwa muda usiojulikana.
"Huyu Mwenyekiti ni jipu maana anatumia mali za ushirika kimabavu na tukihoji tunafukuzwa na akiitisha mkutano mkuu baadhi ya wanachama wanahongwa fedha, ili kupitisha uamuzi ambao wengine wametufukuza na wanachama wengine wamekufa, lakini bado wanatumia majina yetu na marehemu kwenye mikutano kila inayofanyika," alisema.
Baada ya wanaushirika kutoa madukuduku yao, Nasha alimpa nafasi Morobo kujitetea na kukiri kuwa alisafiri kwenda Morogoro kikazi lakini alipofika tu aliambiwa nyumbani kuna mgonjwa kisha alilazimika kurudi.
Kuhusu madai ya fedha za posho, alisema alirudisha ingawa hakusema ni kiasi gani na alipoambiwa na Naibu waziri, Nasha kuwa aonyeshe risiti ya kukabidhi fedha hizo alisema anatoa.
Na alipoulizwa kwa nini aliwafukuza wanachama waliokuwa wanahoji mapato na matumizi, alisema wanakikuka maadili ya chama na pia wanapenda kufanya fujo.
Alizidi kujitetea kuwa wanachama wenzao waliazimia kuwasimamisha kwa muda usiojulikana na ndipo Naibu Waziri alipotoa rai kwa wanachama hao kuwarejesha watakapofanya mkutano hivi karibuni.
Pia Nasha aliwataka Morobo, Masoki na Uroki kurudisha mashamba waliyopeana kinyume cha utaratibu kuagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini kama mwenyekiti huyo hajiingizi katika siasa na ikibainika hivyo, aamue moja kuendesha chama cha ushirika au cha siasa.
Post a Comment