Social Icons

Loading...

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA TAMKO ZITO KWA WAKWEPA KODI... HUYU JAMAA NI NOMA ASEE...EBU SOMA UJIONEE

Katika kuhakikisha serikali inakusanya kodi kikamilifu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema itaendelea kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kodi.
 
Amesema serikali imelenga kukuhakikisha mapato yanaelekezwa katika miradi ili kuharakisha maendeleo ya Watanzania kwa kuwahudumia wananchi.
 
Kauli hiyo aliitoa jana Busega mkoani Simiyu, wakati akihutubia wananchi katika mji wa Nyashimo, baada ya kupokea taarifa  iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa huo, Elaston Mbwilo.
 
“Hii serikali iliyoko madarakani imekuja na mkakati wa kukusanya mapato kwa nguvu zake zote hasa kwa wafanyabishara wakubwa, ambao kwa muda mrefu, wamekuwa wakikwepa kodi na kusababisha serikali kushindwa kuwahudumia wananchi, jambo ambalo sitalikubali nikiwa mtendaji mkuu wa serikali,” alisema.
 
Aliongeza kuwa hawatakuwa na huruma kwa wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kuwa kwa kutokufanya hivyo, serikali itashindwa kutekeleza ahadi zake za kuwahudumia wananchi ikiwamo utoaji wa elimu bure. 
 
Hata hivyo, Majaliwa aliwaondolea wasiwasi wafanyabiashara  waaminifu kuwa serikali haitawabughudhi isipokuwa itapanua wigo kwao wa kufanya biashara na mataifa mbalimbali kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
 
Awali, Mbwilo alisema kutokana na serikali kukusanya mapato yake kutoka kwa wafanyabiasha, mkoa umemokea kiasi cha fedha Sh. Bilioni 1.9 katika kutekeleza utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha nne.
 
“Hadi sasa mkoa wetu wa Simiyu umepokea Sh. bilioni 1.9 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ya awali hadi kidato cha nne. Hii ni kutokana na kasi yake ya kukusanya mapato,’’ alisema.
 
Waziri Mkuu yuko Mkoa Simiyu kwa ziara ya siku tano kukagua  shughuli mbalimbali za maendeleo.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright MAWINGUBONGO
Back To Top